Loading...
title : Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
link : Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
MwambawahabariFrank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali imepanga kuzalisha mitamba zaidi ya milioni 1 kwa mwaka ili kukuza sekta ya mifugo hapa nchini ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari- MAELEZO, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa wananchi.
“Vituo vya uhaulishaji vilivyopo Arusha na Sao Hill Iringa vimeboreshwa ili viweze kutoa mbegu bora za kutosha kwa kufanya maboresho makubwa katika vituo vya kanda vya uzalishaji mbegu za mifugo” alisisitiza Mpina
Amesema kuwa kuelekea uchumi wa viwanda, Serikali imejipanga kuzalisha mifugo mingi ya kutosha ili kupata bidhaa bora zitokanazo na mifugo, Aliongeza kuwa Serikali imevunja mikataba na wawekezaji wengi ambao hawakuweza kutimiza malengo ya uwekezaji katika sekta ya mifugo.
Katika kuboresha sekta ya uvuvi Waziri Mpina amesema wafanyabiashara watumie fursa ya kuzalisha nyavu halali ili kuchochea ukuaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya bidhaa za uvuvi.
Pia aliwaasa Viongozi wote wa Serikali kutojiusisha na uvuvi haramu kwani ni kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Katika kuimarisha sekta ya mifugo amesema kuwa Serikali imeendelea kukusanya madeni yanayodaiwa na NARCO ambapo zaidi ya bilioni 3 zimekusanywa.
Kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinarushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO kikiwashirikisha Mawaziri wote kwa awamu hii.
Hivyo makala Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
yaani makala yote Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/sekta-ya-mifugo-kuchochea-ujenzi-wa_31.html
0 Response to "Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda"
Post a Comment