Loading...
title : SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA
link : SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA
SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amemtaka mkandarasi China Geo- Engineering Corporation aneayejenga barabara ya Mpemba-Isongole KM 50.3 kwa kiwango cha lami kuongeza kasi ya ujenzi ili barabara hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa.
Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza vifaa, wafanyakazi ili ujenzi wake ugawanywe sehemu mbili na hivyo kuwezesha ujenzi huo kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwakani. “Kutokana na umuhimu wa barabara hii kwa uchumi wa mkoa wa Songwe hakikisheni inakamilika ili kufungua uchumi wa Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla”, amesema Mhe, Kwandikwa.
Barabara hiyo ambayo inaunganisha Tanzania na Malawi kupitia mto Songwe itachochea huduma za uchukuzi na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Songwe mhandisi Yohana Kasaini amesema barabara hiyo inahusisha ujenzi wa madaraja makubwa manne, ya kati 14 na madogo 172, imesanifiwa kubeba magari ya aina zote na itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 107 itakapokamilika.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Songwe na hospitali ya Tunduma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA),mkoani Songwe na kumtaka kaimu meneja wa TBA mkoani humo msanifu majengo Christine Shayo kuhakikisha ujenzi huo licha ya kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo hayo pia ukamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.
Zaidi ya kilomita 3,856 za barabara nchini zitasanifiwa ili kujengwa kwa lami katika mwaka wa fedha 2018/2019
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA mkoani Songwe msanifu majengo Christine Shayo, wakati wa ukaguzi wa shughuli za TBA mkoani Songwe .
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe inayojengwa na Wakala wa Majengo Nchini TBA mkoa wa Songwe.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.
Hivyo makala SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA
yaani makala yote SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/songwe-kamilisheni-ujenzi-kwa-wakat.html
0 Response to "SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA"
Post a Comment