Loading...

TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

Loading...
TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA
link : TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

soma pia


TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

 Mradi mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge ulipofikia baadhi ya maeneo.
 Mataaluma yakiwa tayari kwaajili ya kwenda kuwekwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa itapita. 
Maeneo yanayoendelea kujengwa reli ya kisasa eneo la Mlandizi.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya jamii.

*Mkurugenzi Mtendaji Kadogosa asema ujenzi umekamilika kwa asilimia 22
*Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi washuhudia kasi ya ujenzi kuanzia Dar 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa amesema kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta huku akieleza kuna baadhi ya madereva wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma hizo.

Kadogosa amesema hayo leo katika eneo la Soga mkoani Pwani ambapo kuna kambi ya wafanyakazi wanaojenga Reli ya Kisasa ambapo ameelezea namna ambavyo wamedhibiti wizi wa mafuta kwa kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana na mamlaka za ulinzi na usalama.

Sababu za kuelezea hayo ni baada ya baadhi ya waandishi waliokuwa kwenye ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC  wakiongozwa na Mwenyekiti wao Profesa John Kondoro kutaka kufahamu hali kutokana na kuwepo kwa taarifa za uwepo wa wizi wa mafuta.

"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta katika mradi huu.Ni tofauti na hapo awali, tumeimarisha ulinzi na sasa tumefanikiwa kudhibiti wizi huo.

"Kuna watu 30 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mafuta na tayari wamefunguliwa kesi.Pia katika kukomesha vitendo vya wizi kuna baadhi ya madereva ambao tumewafukuza,"amesema Kadogosa.


VIPI KUHUSU UJENZI WA RELI?
Akizungumzia ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ambayo awamu ya kwanza ni kutokea Dar es Salaam hadi Morogoro, Kadogosa amewaeleza wajumbe wa bodi hiyo  kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 22.

Amesema katika ujenzi wa reli hiyo kuna hatua mbalimbali za ujenzi zinazoendelea na kila eneo kwa asilimia tofauti na eneo jingine lakini kwa ujumla wake ujenzi umefikia asilimia 22 na ujenzi unaendelea kwa kiwango cha kuridhisha.

Ameongeza ujenzi wa madaraja unaendelea na tayari zimeanza kuwekwa , ujenzi wa tuta nao unaendelea na maeneo maeneo mengine wameanza kuweka kokoto kwa ajili ya kuanza kutandika mataluma.

"Kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa inakwenda vizuri, ratiba ya ujenzi huu unatakiwa kukamilika Novemba mwaka 2019, hivyo kazi inaendelea na ujenzi unafanyika usiku na mchana na sisi TRC muda wote tumekuwa tukifuatilia tena hatua kwa hatua,"amesema Kadogosa.

Ametumia nafasi hiyo kusisitiza wanafanya kazi kwa saa 24 kwani changamoto ya mvua ilisababisha kutofanyika kazi za ujenzi na hivyo wamemua kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.


UNAZUNGUMZIAJE UJENZI STESHENI YA DAR?
Kadogosa amefafanua kwamba ujenzi wa stesheni ya Dar es Salaam na maeneo mengine ya mradi huo yamezingatia uhalisia wa Mtanzania na kwamba kabla ya kuanza ujenzi huo walimtaka mtalaamu kuonesha ramani ya majengo atakayojenga.

Amesema hata baada ya kuangalia walimtaka ajenge majengo ambayo yataonesha uhalisia wa nchi yetu.Pia amesema maeneo ya Stesheni baada ya kukamilika mbali ya kuwa sehemu ya abiria yatakuwa na maeneo ya mahitaji yote muhimu.


Hivyo makala TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

yaani makala yote TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/trc-wadhibiti-wizi-wa-mafuta-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA"

Post a Comment

Loading...