Loading...
title : UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020.
link : UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020.
UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Burundi kumaliza majadiliano ya kisiasa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ili kuwe na mwafaka na mshikamano na kutaka wahusika wote kushiriki bila kuwepo masharti.
Taarifa ya Baraza hilo imesema Burundi imekuwa katika migogoro tangu Aprili 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kugombea urais kwa awamu ya tatu na hatimaye kushinda nafasi hiyo licha ya kugubikwa kwa maandamano na vurugu.
Kufanikiwa kwa kura ya maoni ya Katiba mpya iliyofanyika Mei mwaka huu ndiko kulikoamsha UN kuitaka Burundi kuweka pia mambo sawa kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Katika kura za maoni, Rais Nkurunziza alipigania hatua hiyo iliyoongeza muda wa rais kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba, wengi wakiamini alikuwa anajitengenezea mazingira ya kuendelea kubaki madarakani, lakini kinyume cha matarajio ya wengi, alitangaza kutogombea urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.
Endapo angetumia mwanya ya Katiba iliyopitishwa, Nkurunziza angeweza kuongoza hadi mwaka 2034 endapo angewania kutetea nafasi yake mwaka 2020.
Kutokana na uamuzi wa Rais huyo kijana wa Burundi aliyeiongoza nchi hiyo kwa takribani miaka 14, Baraza hilo la Usalama limepongeza na kueleza kuwa ni hatua mpya katika kuondoa migogoro ya kisiasa nchini humo.
Hata hivyo, limetaka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, majadiliano ya ndani yatakayohusisha vyama vyote husika ikiwemo vile vya kitaifa, na pia jumuiya za kikanda na kimataifa kuhakikisha mambo yatakuwa sawa.
Ametaka nchi zote katika ukanda wa Afrika Mashariki kusaidia kutafuta suluhu la hali ya kisiasa nchini humo na kujiepusha na kuingiliwa na watu huku wakiheshimu sheria za kimataifa. Baraza la usalama limesema linatarajia uchaguzi ujao utakuwa huru, wenye haki ,wazi ,amani na ushirikishwaji huku ukizingatia haki za kisiasa na binadamu hususan uhuru wa kujieleza. T
akribani watu 180,000 walikimbia nchi hiyo na wengine milioni 3.6 wanaishi kwa misaada huku raia 400,000 wa Burundi wakiishi kama wakimbizi katika nchi jirani.
Hivyo makala UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020.
yaani makala yote UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/un-yaagiza-maandalizi-uchaguzi-mkuu-2020.html
0 Response to "UN YAAGIZA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2020."
Post a Comment