Loading...
title : WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA
link : WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA
WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, amezikumbusha Wizara na Taasisi za Serikali ambazo bado hazijawasilisha mikataba ambayo imeombwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwaajili ya marejejo kufanya hivyo mapema iwezekanavyo.
Ametoa wito huo siku ya jumatano wiki hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka . Uzinduzi huo ulifanywa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Jijini Dodoma.
Akielezea Muundo mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mhe. Waziri Mkuu na majukumu ambayo Ofisi hii imepanga kuyatekeleza. Mwanasheria Mkuu ameyataja baadhi hayo ni pamoja na marejeo ( review) ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya taifa.
“Tumepanga kufanya marejeo ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya taifa. Zoezi hili litahusisha mikataba yote ya kimataifa, mikataba ya uendelezaji madini ( MDAs) na mikataba ya uzalishaji na mauzo ya gesi asilia”, ameeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mikataba mingine itakayofanyiwa marejeo ni mikataba inayohusu uwekezaji baina ya Tanzania na nchi nyingine pamoja na mikataba mingine ambayo Serikali ina maslahi.
“Mhe. Waziri Mkuu, ninaomba kutumia fursa hii kuzishukuru Wizara na Taasisi za Serikali kwa kuendelea kutupatia mikataba tunayoihitaji kufanyia marejeo. Kwa Wizara na Taasisi ambazo hazijawasilisha mikataba iliyoombwa, zinakumbushwa kufanya hivyo mapema ili shughuli hiyo ianze”.Pamoja na kufanya marejeo ya mikataba muhimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Ofisi yake inapanga kuweka mfumo utakaokuwa na regista ya mikataba yote ya kimataifa ili iwe rahisi kuifanyia rejea au kupatikana pindi inapohitajika kwa matumizi mbalimbali ya kiserikali na kisheria.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa maelezo ya muundo mpya ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na majukumu ya Ofisi hiyo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Uzinduzi wa Ofisi hizo tatu ulifanywa na Waziri Mkuu siku ya Jumatano jijini Dodoma ( picha na habari na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) .
Hivyo makala WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA
yaani makala yote WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wasiowasilisha-mikataba-kwa-mwanasheria.html
0 Response to "WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYA HIVYO HARAKA"
Post a Comment