Loading...
title : WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO.
link : WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO.
WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO.
Wadau mbalimbali wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa katika hafla ya kupokea cheti cha kutoa huduma bora za Kimataifa (ISO) iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiimba nyimbo ya kusherekea kupata cheti cha ISO.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Serikali ipo katika utekelezaji wa kuhakikisha kila mtanzania anajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao utamwezesha mwanachama kupata matibabu kipindi ambacho atakuwa mgonjwa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea cheti cha kutoa huduma bora Kimataifa (ISO) kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa serikali itahakikisha watanzania wanakuwa bima ya afya.
Ndugulile amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikosa fedha za matibabu na kushindwa kumudu gharama.
Amefafanua kuwa lengo la serikali ni kufikia asilimia 50 ya watanzania ambao ni wanachama wa NHIF, kwani kwa sasa wapo asilimia 30.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kufikia malengo hayo NHIF inatakiwa kufungua wigo kwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya.
Katika hatua nyengine ameipongeza NHIF kwa kupata cheti cha ISO kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa viwango vya ubora kimataifa.
"NHIF ni taasisi ambayo imekuwa ikifanya maboresho kila wakati jambo ambalo kwa sasa limeleta mafanikio makubwa" amesema Dkt. Ndugulile.
Katika kuboresha utendaji Dkt. Ndugulile amewataka watendaji NHIF kutokaa ofisini muda wote, badala yake kuwafata wananchi katika vituo vya afya kwa ajili ya kuhamasisha wajiunge na mfuko wa bima ya afya taifa.
"Tunapaswa kuongeza vifurushi vya huduma za NHIF ili kuwapa fursa vijana ambao wapo mtaani hawana kazi na wanapenda kwa wanachama ili wapate huduma ya Afya" amesema Dkt. Ndugulile.
Amesema kuwa sekta ya Afya imebadilika sana, hivyo NHIF inatakiwa kutoa huduma za afya kulingana na maitaji kwa sasa.
"Cheti hicho ni hatua kubwa, ambacho kimepatikana kupitia misingi ya utoaji bora za huduma ya Afya" amesema Dkt. Ndugulile.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda, amesema kuwa jambo la muhimu ni kuhakikisha shirika kuwa na sifa za kimataifa.
Amesema kuwa suala la kuwa na viwango bora vya huduma tumefanikiwa kulipa kipaombele ili hukakikisha tunafikia malengo.
"Ifike mahali tunatakiwa kuwa na mfuko ambao utakuwa unatoa huduma bora kwa viwango vya kimataifa" amesema Makinda.
Amesema kuwa kupitia cheti hicho watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora katika vituo vyote vya bima ya Afya.
"Tunategemea kila mtanzania atapata huduma bora za Afya pamoja na kutengeneza mazingira rafiki ya kujiunga mfuko wetu" amesema Anne.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga, amesema kuwa kupata cheti hicho kimetoka na uimara wa utendaji wao.
Amesema kuwa wataendelea kuboresha utendaji wao kwa kuongeza ufanisi ili kuhakisha mipango ya utendaji kazi inafikia malengo.
"Watoa huduma wanatakiwa kuwa waminifu jambo ambalo litasaidia kupiga hatua katika kufikia malengo yetu" amesema Konga.
Hivyo makala WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO.
yaani makala yote WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/watanzania-wote-kupata-bima-ya-afya.html
0 Response to "WATANZANIA WOTE KUPATA BIMA YA AFYA, NHIF YAPATA CHETI CHA ISO."
Post a Comment