Loading...
title : Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena
link : Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena
Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena
Na Andrew Chale, Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtembelea na
kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi
Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha
Taasisi ya mifupa MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili jijini
Dar es Salaam kwa mara nyingine tena.
Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa Kikwete kumtembelea Dk
Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti 8,2018
alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa Matibabu
ya awali na juzi Agosti 15,2018 katika wodi ya Taasisi ya
Mifupa MOI.
Akiwa hospitaini hapo mapema jana, Kikwete ameweza
kumjulia hali na kubadilishana nae mawazo mbalimbali
huku akimtakia unafuu aendelee na majukumu yake ya kila
siku na akimpongeza kwa shughuli zake anazozifanya katika
kuinua sekta ya Utalii pamoja na kulinda rasilimali za
Maliasili.
“Nikutakie kheri. Nashukuru kwa kukuta unaendelea vizuri
sasa na nilikuja ukiwa upo unaongea ukiwa umelala
kitandani na kwa sasa nimekuja tena umeweza kuimarika na
hata kutembea na kukaa kama hivi hongera sana” alieleza
Kikwete wakati akimjulia hali Waziri Kigwangalla wodini
hapo.
Tayari jopo la Madaktari bingwa wa MOI wamebainisha
kuwa Dkt. Kigwangalla kwa sasa anaendelea vizuri na muda
wowote anaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani ambapo kwa
sasa sehemu zilizobakia ni mkono wake wa kushoto ambao
kila siku unaendelea kuimarika.
Hata hivyo, Dkt. Kigwangalla amemweleza Kikwete kuwa
kwa sasa hali yake inaendelea kuwa vizuri na muda wowote
anaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani huku akiendelea na
mazoezi kidogokidogo.
Aidha, jioni ya jana Dkt. Kigwangalla ameweza kufanya
mazoezi ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa moja
kuanzia kwenye viunga vya Hospitali hiyo na kuzunguka
maeneo yanayozunguka Muhimbili na baadae kupanda kwa
kutumia ngazi katika jengo anapopatiwa matibabu kwa
miguu mpaka gorofa ya sita.
Waziri Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti
4, 2018 huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo
katika ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, Afisa Habari wa Wizara
hiyo Hamza Temba alifariki dunia huku watano
wakijeruhiwa akiwemo yeye anaendelea na matibabu
Hospitalini hapo.
Hivyo makala Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena
yaani makala yote Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-dkt-kigwangalla-fiti-kurejea.html
0 Response to "Waziri Dkt Kigwangalla 'Fiti' Kurejea Nyumbani ,Kikwete Amtembelea Tena"
Post a Comment