Loading...
title : WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI
link : WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI
WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga katika kukagua utekelezaji wa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na hakuridhishwa na utendaji wa baadhi ya wahusika katika idara hizo na kuamua kuwaweka kando ili wenye kasi watekeleze jukumu hilo.
Katika Ziara hiyo Kalemani amemuagiza meneja Tanesco mkoa wa Pwani kumsimamisha kazi Mhandisi wa Mkoa na pia amemuagiza meneja wa wilaya ya Mkuranga Mhandisi, Regina Mvungi kumsimamisha mhandisi mwenye dhamana hiyo katika wilaya ya Mkuranga kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyo kwenye mradi kata ya Vikundi.
Aidha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 Wilayani Mkuranga katika kuhakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vilivyokatika mpango huo.Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikindu na Tambani.
Kalemani amesema kuwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya pili haikufanya vizuri katika Tarafa ya Kisiju hivyo natoa siku 14 kuanzia kesho kuhakikisha umeme unawaka, aidha Kalemani ametoa maagizo kwa viongozi wa Tanesco katika ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha umeme huo unawaka kwa wakati.
Naye Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega amesema wananchi katika vijiji ambavyo vilitakiwa kupata umeme walikata minazi na miembe yao ili kupisha miundo mbinu ya umeme lakini ni zaidi ya miaka mitano tangu miundombinu ya umeme iwekwe na hakuna umeme.
Aidha Ulega amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni hapo kwani anaamini italeta mabadiliko na amewataka watendaji waliopewa maagizo na Waziri wayafanyie kazi mara moja.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani(katikati)kwa kushiriki na viogizo mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika kijiji cha Mkokozi Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (alienyosha mkono) akizungumza na wanachi wa kata ya Kisiju wilaya ya Mkuranga ambapo amewaagiza watendaji wa Tanesco siku 14 wahakikishe umeme umewaka (Picha Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI
yaani makala yote WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-kalemani-awasimamisha-kazi.html
0 Response to "WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI"
Post a Comment