Loading...
title : WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI
link : WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI
WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini.
Lugola alisema hayo baada ya kulikagua Gereza jipya la Wilaya ya Ruangwa linalojengwa ambalo lina ekari 100 lakini ekari 20 limevamiwa kwa kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ufuta na korosho katika eneo hilo la Jeshi la Magereza.
Akizungumza baada ya kulikagua Gereza hilo, mjini Ruangwa leo, Lugola alisema kuanzia sasa viongozi wa vyombo vyake wahakikishe hawaruhusu mwananchi yeyote kuingia katika maeneo ya jeshi na atakua mkali kulifuatilia suala hilo.
Lugola ambaye pia aliikataa kuipokea taarifa ya ujenzi wa gereza hilo ambayo ilikua inasomwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Rajabu Nyange, alisema taarifa hiyo ina upungufu mkubwa na hawezi kuipokea licha ya kua imeeleza kuhusu ardhi ya jeshi hilo kuvamiwa.
“Mimi huwa nashangaa sana inakuaje wananchi wanavamia ardhi ya jeshi tena bila woga, halafu jeshi linakaa kimya linabaki kunung’unika, hii haijakaa sawa kabisa na kamwe sikubaliani nalo,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kua, “uvamizi wa ardhi mara nyingi unakua kwa jeshi la polisi na magereza, mbona Jeshi la Wananchi silisikii hili, kwanini nyie mnakaa kimya wananchi wakivamia ardhi yenu, sasa nawataka muhakikishe ardhi ya jeshi popote nchini iliyoporwa inarudishwa ndani ya jeshi, na wote waliovmia waondooeni haraka iwezekanavyo.”
Hivyo makala WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI
yaani makala yote WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-lugola-aitaka-polisi-magereza.html
0 Response to "WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI"
Post a Comment