Loading...

WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC

Loading...
WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC
link : WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC

soma pia


WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC


*Ni baada ya walimu kumtuhumu kwa ulevi, rushwa, kughushi nyaraka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Bibi. Pudencis Protas kumkamata Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wa wilaya ya Ruangwa Bw. Anthon Mandai kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walimu wakimlalamikia kiongozi huyo kuwa na tabia za kudai rushwa, kutowapandisha madaraja, ulevi pamoja na kuwaita walimu hao kwenye vilabu vya pombe kwa ajili ya kuwasikiliza matatizo yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Agosti 12, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika siku ya mwisho ya ziara kyake ya kikazi wilayani hapa. Bw. Mandai anakaimu nafasi hiyo tangu Juni, 2012.

Amesema mbali na kulalamikiwa na walimu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ulevi na kuwaita walimu katika vilabu vya pombe pindi wanapohitaji kuhudumiwa, pia amekuwa akighushi nyaraka za mirathi, jambo linalosababisha baadhi ya familia za waliokuwa walimu kuchelewa kupata haki zao.

“Huyu Katibu ameshindwa kuwasaidia walimu katika kutatua changamoto zao na badala yake amekuwa akitumia vibaya majina ya viongozi wakuu, ambapo hata mimi alijaribu kutaka kunichakachua kwa kughushi muhtasari wa kikao cha mirathi ya Mwalimu Suwedi Chikawe akitumia jina langu kuwa nilikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa na agenda ya kumbadilisha msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na familia jambo ambalo si la kweli,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Fadhili Juma, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Anthon Mandai, akipanda gali la Polisi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudencis Protas, kumkamata ili akajibu tuhuma zinazomkabili, Agosti 12.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .



Hivyo makala WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC

yaani makala yote WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-mkuu-amuagiza-rpc-lindi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC"

Post a Comment

Loading...