Loading...
title : TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO
link : TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO
TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO
Na. Jeshi la Polisi.
Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) imemalizika Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la Polisi nchini likishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza imeenda Kenya na ya tatu Uganda.
Polisi Tanzania imeshika nafasi hiyo baada ya kuchukua jumla ya Medali 64, 15 za dhahabu, 25 za fedha na 24 za shaba huku Kenya ikiwa na medali 68, 25 dhahabu , fedha 20 na shaba 24.
Mshindi wa Tatu Uganda alijinyakulia Medali 36, Rwanda 27, Burundi nane, Sudani Kusini sita na Sudani moja ambapo timu za Polisi Tanzania zimetwaa ubingwa katika Soka, Mpira wa pete, Judo, na Kulenga Shabaha kwa upande wa Wanaume.
Akifunga Michezo hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Wanamichezo hao kudumisha umoja na Amani katika mataifa wanayotoka ikiwemo kutumia michezo hiyo kubadilishana mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu.
Aliwapongeza Wanamichezo wote walioshiriki michezo hiyo kwa kuonyesha nidhamu na ushindani wa hali ya juu jambo ambalo limefanya michezo hiyo kuvutia watazamaji wengi.

Wanamichezo wa Polisi Tanzania walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufungaji wa michezo hiyo (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wanamichezo wa Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi kombe la mshindi wa tatu nahodha wa timu ya mbio ya Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Rwanda akimkabidhi Kombe la mshindi wa Pili katika kulenga Shabaha Inspekta wa Polisi Tannzaia wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya akimkabidhi kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu Inspekta Hashim Abdalah kutoka Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi). KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO
yaani makala yote TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/tanzania-ya-pili-michezo-ya-eapcco.html
0 Response to "TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO"
Post a Comment