Loading...
title : AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI
link : AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI
AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani[CCM akizungumza katika mkutano wa hadhara eneo sokoni wilayani Pangani kabla ya kushuhudia utiliaji wa saini ya mkataba wa maji kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo baina ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) wilayani hapo.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemtaka mkandarasi toka Kampuni ya Macarious Hotela and Co.Ltd ya Jijini Tanga kumaliza mradi wa maji katika mji wa Pangani wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500 kwa wakati kabla ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu.
Aweso ambae pia ni Mbunge wa Pangani ameyasema hayo wakati wa zoezi la kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo baina ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) Wilayani hapo.
“kwa kweli hatuta kuwa na msamaha kwa Mkandarasi atakae kwenda kinyume na matakwa ya utekelezaji wa mradi huu kama yalivyoainishwa katika mkataba tutakuwa wakali kweli”Alisema Aweso.
Aidha alisema mradi huo utawanufaisha wananchi wa Pangani Mashariki na Magharibi ambapo unatarajiwa kutekelezwa ndani ya kipindi cha miezi kumi kama makubaliano yalivyoafikwiwa na pande mbili upande wa Serikali na Mkandarasi.
Alisema Wizara hiyo ya Maji na Umwagiliaji imetenga fedha hizo ili kutatua kero za wananchi wa maeneo hayo hivyo Serikali haitakuwa na uvumilivu na mkandarasi atakae kwamisha jitihada hizo za Serikali.
Hivyo makala AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI
yaani makala yote AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/aweso-amtaka-mkandarasi-wa-mradi-wa.html
0 Response to "AWESO AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI KUUMALIZA KWA WAKATI"
Post a Comment