Loading...
title : DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI
link : DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI
DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wameendelea kuboresha huduma ya maji sehemu mbalimbali ikiwemo kuongeza maji ya kutosha katika bandari ya Dar es Salaam.
Mkakati huo umeanza kutekelezwa rasmi na Mkoa wa Dawasa Ilala kwa kuanza zoezi maalum la kuunga Bomba kubwa la kipenyo nane ili kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini.
Meneja wa mkoa Ilala Judith Singinika amesema kuwa zoezi linatekelezwa kulingana na agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa alilolitoa alipotembelea mamlaka hiyo ya Bandari.
Amesema kuwa, kukamilika kwa zoezi la kuunga bomba hilo kutaongeza wingi wa maji katika bandari hiyo ya Dar es salaam na kuhakikisha kuwa mahitaji ya huduma ya maji kwenye eneo lote la Bandari yanafikiwa.
Aidha kazi hii itawezesha pia meli zote za abiria na mizigo zinazotia nanga katika bandari hii kibwa kuliko zote nchini zinapata maji safi na kukidhi mahitaji.
Hapo awali, Bandari walikuwa wananunua maboza kutoka nje kwa ajili ya matumizi ya meli zinazotia nanga na Profesa Mbarawa alipiga marufuku na kuwataka watumie maji ya Dawasa kwa usalama zaidj.
Kazi hii ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.
Ujenzi wa kuunga bomba kubwa la maji lenye kipenyo nane ili kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini ukiendelea kufuatia agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.
Hivyo makala DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI
yaani makala yote DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/dawasa-waanza-ujenzi-wa-bomba-kubwa-la.html
0 Response to "DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI"
Post a Comment