Loading...
title : Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini
link : Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini
Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini
Na Mwandishi Wetu.
Serikali imewahimiza wafanyakazi kote nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujiletea maendeleo na kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokuwa akiongea na viongozi wanawake wa Mkoa wa Morogoro kutoka vyama vya wafanyakazi ikiwemo TAMIKO, CWT, TUICO, TALGU, TULGE, TPAWU na CHODAWU.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imelenga kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kwa kuhakikisha wanashirikishwa kwenye dhana ya uchumi wa viwanda. Lengo likiwa ni kuwawezesha wafanyakazi wanashiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa kwa kufuata kanuni na taratibu ya dhana nzima ya uchumi wa viwanda.
"Mnao uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na mkawa chachu ya maendeleo ya viwanda kwenye uchumi wa taifa letu, kwa kuweza kutoa ajira, vilevile kuwasaidia ninyi kupiga hatua za maendeleo kwa kufanya kazi kwa uzalendo na weledi kwa kutumia sera ya viwanda" ameeleza Waziri Mhagama.
Aidha, aliongeza kuwa, Sera ya uchumi wa viwanda iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ni jambo jema linalolenga kuboresha maisha ya watanzania.
“Mheshimiwa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza azma ya kujenga Tanzania ya viwanda, hivyo nitafurahi sana kama Waziri mwenye dhamana ya wafanyakazi kuhakikisha tunaleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa wafanyakazi.” Alisema Mhagama.
Alitoa rai kwa viongozi wanawake kuhakikisha wanaratibu na kusambaza ujumbe huu wenye habari njema kwa wanawake nchi nzima waliopo kwenye sekta ya ajira kuchangamkia fursa hii kwa kuanzisha miradi mbalimbali itakayowawezesha kuwakomboa kiuchumi.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa alifafanua juu ya sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambayo imelenga kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitaji ili kuwawezesha wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Viongozi wanawake kutoka vyama vya wafanyakazi Mkoani Morogoro kuhusu kuwahimiza wafanyakazi kuchangamkia fursa za shughuli za kimaendeleo zilizopo nchini.
Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamuhoke akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana kwa lengo la kuzungumza na Viongozi Wanawake kutoka kwenye Vyama vya Wafanyakazi Mkoani Morogoro.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumzia Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa viongozi kutoka vyama vya wafanyakazi walipokutana Mkoani Morogoro.
Baadhi ya viongozi kutoka kwenye Vyama mbalimbali vya Wafanyakazi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana nao kuzungumzia ushirikishwaji wa wafanyakazi kwenye dhana ya uchumi wa viwanda.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini
yaani makala yote Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/serikali-kuleta-mabadiliko-ya-kiuchumi.html
0 Response to "Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini"
Post a Comment