Loading...
title : DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU.
link : DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU.
DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema amewataka wananchi wa Mtaa wa kimanga waliojenga karibu na mto tenge kukutana naye katikamkutano wake ambao anatarajia kuufanya mwishoni mwezi huu kwajili ya kujadiliana kuhusu kupisha upanuzi wa mto huo kwa kuwa namafuriko wakati wa mvua.
DC Mjema ameyasemahayo alipokuwa akikagua barabara ya kimanga darajani na mto tenge na kujionea jinsi watu walivyo jenga karibu na mto huo jambo ambalo limesababisha mto huo kujaa mchanga na taka taka na kuongeza hatari ya mafuriko wakati wa msimu wa mvua.
Katika hatua nyingine DC Mjema amemwagiza mhandisi wa TARURA Manispaa ya Ilala kuhakikisha anasimamia ujenzi wa barabara ya Kimanga Mazda ili iweze kukamilika haraka ifikapo mwezi Machi 2019 ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuondokana na adha ya usafiri.
"Naomba mfikishie salamu zangu huyo mhandisi anaye jenga hii barabara fedha tumeshampa nataka afanye ujenzi ujenzi huu haraka na mimi nitafuatilia mpakanione amekamilisha, nanyi wananchi tusaidieni mlipe kodi ya serikali kwa wakati ilituweze kutekeleza miradi hii mapema maana ujenzi ulikwama kwa kuwa hatukuwa nafedha za kumlipa laikini sasa tumelipaa nafedha zipo" alisema.
Pamoja na hayo Mjema amewataka wananchi wanaoishi katika eneo la Kisukuru karibu na daraja linalotenganisha Maispaa ya Ilala na Ubungo kuacha kugomea eneo hilo badala yake wafuate utaratibu na kuwaambia kuwa eneo hilo kwa sasa kisheria linasomeka liko manispaa ya Ilala na kwa kuwa linaonekana kuwa na mgogoro wawe na subira kwani amelifikisha kwa Waziri wa Ardhi na anasubiri majibu na na uamuzi.
''Kuna serikali moja tu hatuna serikali nyingine nawaambia nyie mno leta vurugu hapa muache kama wewe unataka kuishi ubungo hujakatazwa hamia tu acha fujo ,mtendaji wewe unayo mamlaka ukiona mtu analetafujo wekandani lazima tuheshimu Sserikali" alisema .
Wananchi wa Kimanga na Kisukuru wakiwasilisha kero zao mbele ya mkuu wa Wilaya wameomba ,kuboreshewa huduma za Afya ,Maji ,Barabara na Umeme .
Hivyo makala DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU.
yaani makala yote DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/dc-mjema-azungumza-na-wananchi.html
0 Response to "DC MJEMA AZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOJENGA KANDOKANDO YA MTOTENGE ,AONYA WANAOGOMBEA MPAKA KISUKURU."
Post a Comment