Loading...
title : DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM
link : DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM
DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Zimbabwe anayekipiga sasa hivi katika Kikosi cha Azam Donald Ngoma, amerejea tena dimbani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Ngoma aliyesajiliwa Azam msimu wa 2018/19 akitokea Yanga amekaa nje ya Uwanja toka ligi kuanza akiwa anauguza majeraha ya muda mrefu aliyoumia akiwa anaitumia klabu yake ya zamani.
Azam jana ilikuwa katika Uwanja wake wa nyumbani Azam Complex wakiikaribisha Lipuli na kutoka suluhu, na kushuhudia mshambuliaji huyo akicheza kwa mara ya kwanza toka asajiliwe na timu hiyo kutokea Yanga. Ngoma alifanikiwa kuingia katika kipindi cha pili dakika ya 62 kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Mudathir Yahya na
Licha ya kutoka kwenye majeraha ya takribani mwaka mmoja, Ngoma alionekana kuanza vema jana mechi yake ya kwanza akicheza kwa kujituma na kupambana kwenye dakika zote.Kwa upande wake binafsi baada ya kumalizika kwa mchezo huo jana, Ngoma amefurahia sana kurejea tena uwanjani baada ya kutoka kwenye majeruhi licha ya timu yake kutopata ushindi dhidi ya Lipuli.
“Azam imenifanyia vitu vikubwa sana na mimi nimefurahi sana kuwa hapa, kuvaa jezi ya Azam, ni kitu kizuri na nimefurahi sana kwa mechi yangu ya kwanza, nafikiri tunatakiwa kuchukua pointi zaidi,"“Tunakiwa kushinda mechi zaidi hususani mechi za nyumbani, tunatakiwa kupata pointi zinazohitajika, nafikiri tunatakiwa kujiboresha tunatakiwa kufanya vizuri zaidi, tunatakiwa kushinda haswa mechi za nyumbani,” alisema.
Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe, aliwapa tano mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa wamekuwa wakiwapa sapoti mwanzo mwisho licha ya kutowafurahisha katika mchezo huo.“Mashabiki wamekuwa wakifanya kazi nzuri unajua wamekuwa wakijaribu kutusukuma kila mara kwa bidii hata pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri hususani mechi ya leo tulitakiwa kuwapa furaha lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hivyo lakini nawaahidi mambo mazuri yanakuja,” alisema.
Mshabuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe anayekipiga Azam Donald Ngoma (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Lipuli Novat Lufunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliochezwa jana usiku na kumalizika kwa timu hizo kutoka Suluhu ya 0-0.
Hivyo makala DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM
yaani makala yote DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/donald-ngoma-rasmi-aanza-kuitumia-timu.html
0 Response to "DONALD NGOMA RASMI AANZA KUITUMIA TIMU YAKE YA AZAM"
Post a Comment