Loading...

SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA

Loading...
SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA
link : SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA

soma pia


SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Limemtangaza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) kati ya Simba na Yanga.

Simba na Yanga zinakutana kesho katika mchezo wa Ligi kuu kuanzia majira ya saa 11 jioni ukiwa ni mchezo uliosubiriwa kwa muda mrefu.

TFF wametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wao wakimtangaza Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo ya watani wa jadi huku viongozi mbalimbali nao wakitarajia kuja kushuhudia mchezo huo.

Simba na Yanga zinakutana kesho katika Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa ni mara ya 93, Yanga akishinda mara 34 na Simba mara 26 huku wakitoka sare mara 30.Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini utakuwa wa kusisimua kwa kila upande kutaka kuibuka na ushindi.

Mitaani kumekuwa na tambo mbalimbali kutoka kwa mashabiki, kila upande wakisifia kikosi chao kwa upande wa Simba wenye alama 10 baada ya kucheza mechi 5 watashuka dimbani bila mshambuliaji wao John Bocco anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu lakini wakiwa na washambuliaji wengine Kama Meddie Kagere, Emanuel Okwi, Marcelo Kaheza na Adam Salama. 

Kwa upande wa viungo Simba wamekuwa na muunganiko mzuri kutoka Jonas Mkude, James Kotei, Mohamed Ibrahim, Clatous Chama na Shiza Kichuya huku mabeki wao Pascal Wawa, Mohamed Hussein, Shomar Kapombe na Erasto Nyoni wakitegemea kupewa nafasi kubwa ya kulinda lango lao linalindwa na Aishi Manula.

Yanga wenye alama 12 baada ya kucheza michezo minne kwa upande wao wana kikosi chenye wachezaji wengi wachanga akiwemo beki wa kulia Paul Godfrey, Gadiel Michael akicheza kushoto kati wakiwa na Kelvin Yonda sambamba na Dante na kwa upande wa viungo Yanga wamekuwa na idadi nzuri ya wachezaji wa kati ila katika mechi nne zilizopita Papy Tshimbimbi na Feisal Salum "Fei Toto' wamekuwa wanaanza pamoja ikiwemo na Deus Kaseke na Mrisho Ngasa.

Kwa upande wa washambuliaji Yanga wamekuwa wanatumia mipira mirefu kutoka kwa Ibrahim Ajib aliyeonesha uwezo mkubwa sa a akifunva goli moja na akitoa nafasi za goli nne akiwa na Heritier Makambo na Amis Tambwe aliyecheza mchezo wake wa Kwanza dhidi ya Singida na kufanikiwa kufunga goli 2 ila katika nafasi ya golikipa Yanga haijawa na uhakika wa nani anayeanza ila Beno Kakolanya anapewa nafasi kubwa baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya Singida 

Kwenye mchezo wa msimu timu hizo zilicheza jumla ya mechi tatu, Mbili zikiwa za Ligi ambapo Simba alifanikiwa kushinda mchezo moja kwa goli 1-0 likifungwa na Erasto Nyoni, mchezo mmoja wakitoka sare 1-1 magoli yakifungwa na Shiza Kichuya kwa upande wa Simba na Obrey Chirwa akisawazisha. Mchezo mwingine ni Ngao ya Jamii Simba wakishinda kwa mikwaju ya penati baada ya kumalizika kwa dakika 90.

Yanga waliokuwa wameweka kambi yao Mji kasoro bahari Morogoro na Simba hapahapa Jijini Dar es Salaam zitashuka dimbani kutafuta nani zaidi.


Hivyo makala SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA

yaani makala yote SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/spika-job-ndugai-mgeni-rasmi-simba-vs.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI SIMBA VS YANGA KESHO TAIFA"

Post a Comment

Loading...