Loading...
title : GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI
link : GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI
GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI
Na Veronica Simba – Dodoma
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema kuwa gesi asilia inayopatikana nchini, ingali na nafasi kubwa ya kuchangia katika Pato la Taifa, tofauti na hofu ya baadhi ya watu kuwa Serikali haiipi tena kipaumbele sekta hiyo.
Alitoa kauli hiyo jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma, wakati akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walizoziwasilisha katika semina maalum iliyoandaliwa na Wizara kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi asilia.
Awali, wakitoa maoni na hoja mbalimbali wakati wa semina hiyo, baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, walionyesha wasiwasi wao kuwa Serikali hailipi tena kipaumbele suala la gesi asilia kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.
“Serikali haijabadili msimamo na mtazamo wake kuhusu gesi asilia hata kidogo. Ndiyo maana Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepewa dhamana ya kufanya kazi kibiashara ambapo pamoja na mambo mengine, linashughulika na biashara ya gesi ili kukuza mchango wake katika Pato la Taifa,” alifafanua Naibu Waziri.
Akifafanua zaidi, alisema kwamba, miradi mbalimbali ya gesi asilia inaendelea hivi sasa ambayo ni pamoja na uunganishaji wa gesi katika kiwanda cha saruji cha Dangote, katika viwanda vikubwa vilivyopo Mkuranga pamoja na kuunganisha majumbani.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akizungumza wakati wa Semina ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani), kuhusu masuala ya umeme, mafuta pamoja na gesi. Semina hiyo ya siku mbili iliandaliwa na Wizara ya Nishati ambapo ilihitimishwa jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma.
Meza Kuu – Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula na Kaimu Katibu wa Kamati Agnes Nkwera, wakiwa katika Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani), kuhusu masuala ya umeme, mafuta pamoja na gesi. Semina hiyo ya siku mbili ilihitimishwa jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakichangia hoja na kutoa maoni wakati wa Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu masuala ya umeme, mafuta pamoja na gesi. Semina hiyo ya siku mbili ilihitimishwa jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kuhusu masuala ya umeme, mafuta pamoja na gesi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwemo Wabunge, Viongozi na Maafisa waandamizi kutoka Serikalini, wakiwa katika Semina hiyo ya siku mbili ambayo ilihitimishwa jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma.
Hivyo makala GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI
yaani makala yote GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/gesi-bado-ina-nafasi-kubwa-katika.html
0 Response to "GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI"
Post a Comment