Loading...

Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini.

Loading...
Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini.
link : Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini.

soma pia


Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini.



Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo akizungumza na wandishi wa habari.
Paschal Dotto-MAELEZO
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mionzi (Radiolojia) imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 3.96 kwa kuanzisha huduma ya kutibu wagonjwa wenye uvimbe kwa kutumia vifaa vya mionzi huduma ambayo awali haikuwepo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo, amesema kuwa kupitia huduma hiyo ambayo ilianza rasmi Oktoba mwaka jana mpaka sasa wagonjwa 45  wametibiwa.
“Kabla ya kuanzishwa kwa huduma hii wagonjwa wengi walikuwa wakienda nje ya nchi hasa India ambapo walikuwa wanalipa gharama kubwa sana, lakini kwa sasa huduma hii inapatikana hapa nchini kwa hiyo watanzania wenye matatizo ya uvimbe waje wapate huduma hii kwa gharama nafuu ya milioni 2 kwa kila awamu”, alisema Dkt Ogweyo.
Dkt. Ogweyo alibainisha kuwa kati ya wagonjwa 45 waliotibiwa wamegharimu kiasi cha shilingi milioni 360 tofauti na kupata huduma hii nje ya nchi ambayo ingeweza kugharimu takriban shilingi bilioni 4.320.
Aidha, Dkt. Ogweyo aliongeza kuwa huduma hii inahusisha utaalam wa vifaa vya mionzi (Radiolojia) kama vile X-Ray, MRI, CT- Scan na Ultra-Sound kutibu kabisa ugonjwa au kuchukua sampuli kwa uchunguzi zaidi.
Akiainisha huduma ambazo zinatolewa mpaka sasa na kitengo hicho, Dkt. Ogweyo alisema ni pamoja na kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingo (Haemogioma na Lymphongioma), kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mikojo imeziba, huduma ya kuzibua mirija ya uzazi na kunyonya usaha kwenye uvimbe ulioko tumboni.
Dkt. Ogweyo alibainisha  kuwa kabla ya huduma hii wagonjwa wenye matatizo hayo iliwalazimu kwenda kutibiwa India kwa gharama kubwa zaidi ya shilingi  milioni 96 kwa mgonjwa mmoja lakini kwa hapa nchini ni shilingi milioni 8 tu.
Naye Mkuu wa Idara ya Radiolojia, Dkt. Flora Lwakatale amaipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuanziaha huduma hii nchini.
“Ni furaha na fahari kubwa kwa nchi yetu kwa kuweza kuanzisha huduma hii nchini, naipongeza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweka juhudi katika hili, nawakaribisha watanzania wote tupo tayari kutoa huduma ya matibabu hayo”, alisema  Dkt. Lwakatale.
Kwa upande wao wanufaika wa huduma hii Leyla Maulid na Joan Nico wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuboresha huduma za afya nchini.


Hivyo makala Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini.

yaani makala yote Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/muhimbili-yaokoa-bilioni-396-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Muhimbili Yaokoa Bilioni 3.96 kwa Wagonjwa wa Uvimbe Kutibiwa Nchini."

Post a Comment

Loading...