Loading...

Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa

Loading...
Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa
link : Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa

soma pia


Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa



Hussein Ndubikile, 
Mwambawahabari
Ikiwa imebaki siku moja dunia kuadhimisha Siku ya Afya ya Mazingira jamii imeshauriwa  kuyatunza na kuyahifadhi mazingira ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko yatokanayo kushindwa kuviweka vyakula katika mazingira ya usafi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafi ya ya Kajenjere Trading Company ltd, Mathew Amwali wakati wa shughuli ya ufanyaji usafi katika Soko la Buguruni uliofanywa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara, viongozi wa soko na wadau wa usafi.

Amesema kutokana na jamii kutozingatia kanuni na sheria za usafi wa mazingira huchangia kutokea magonjwa ambukizi yakiwemo ya Kipindupindu, kuhara huku akibainisha takataka zinaweza kutumika njia ya kujipatia kipato.
“Takataka ni fursa ya kujipatia kipato mtu akiweza kuzitenganisha sio kuzichanganya mfano chuma, karatasi  na maboksi  taka zitokanazo na mahindi, mbogamboga  zinaweza kuzalisha molea ya samadi, “ amesema.

Amebainisha kuwa kampuni yake inaunga mkono kauli ya Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda ya kuhakikisha jiji linakuwa katika hali ya usafi na kwamba wako tayari kuzoa taka usiku ili kuondokana na adha ya msongamano muda wa asubuhi na mchana.

Amesisitiza kuwa kauli mbiu ya maadhimnisho hayo ni Usalama wa Chakula kwa afya ya Jamii na uchumi wa viwanda kwa taifa na kueleza kuwa elimu inatakiwa kutolewa kupunguza uchafu wa mazingira.

Kwa upande wake Ofisa Afya wa Mazingira wa Soko hilo, Patrick Mazengo amesema hali ya usafi sokoni hapo imeimarika tofauti na awali ilivyokuwa hivyo wataendelea kuhamasisha usafi wa mazingira kwa wafanyabiashara.
Kwa upande wake Ofisa Afya wa Manispaa ya Ilala, Fatuma Maduhu amesema manispaa hiyo itahakikisha wananchi wake wananshiriki kikamilifu katika shughuli za ufanayaji usafi wa mazingira ili kujiepusha na magonnjwa.  

Mfanyabiashara wa Soko hilo, Rashid Kawangwa amefafanua kuwa wamehamasika kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya soko hilo na kwamba ni endelevu.


Hivyo makala Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa

yaani makala yote Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/jamii-yashauriwa-kuyatunza-na-kuhifadhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa"

Post a Comment

Loading...