Loading...
title : DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI
link : DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI
DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI

Na John Luhende
Mwambawahabari
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Sarah Msafiri ameitaka wakala wa ufundi na umeme TEMESA katika Kivuko cha Magogoni kushirikiana na wadau wadau kutoa elimu ya uokoji kwa abiria ikiwemo matumizi ya Vifaa vya uokozi maboya na lifejacket.

DC Msafiri ameyasemahayo leo katika ziarayake ya kushtukiza kukagua huduma za Kivuko hicho, na kuagiza kufungwa camera za usalama, TV za kutoa elimu namna ya kujiokoa kwa kutumia mamboya wakati wa dharula, kuwa na namba ya simu ya dharula ndani ya wiki moja wasipo tekeleza atakifunga kivukohicho.

"Sijaridhika na usalama wa Kivuko hiki kunamabo mnayaona madogo lakini yanaweza kuhatarisha maisha ya abiria mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama sitakubali wananchi wangu yawakute Nita rudi hapa tarehe 4 Oktoba nikikuta hamjayarekebisha ntakifunga Kivuko ili watu wapite darajani "alisema
Aidha DC Msafiri ameitaka TEMESA kuzishirikisha taasisi za Serikali zinashughulika na mambo usalama Zimamoto, Polisi Marine na Jeshi la maji Kigamboni NAV katika kuelimisha abiria wanaotumia Kivuko hicho.
Kwa upande wake Katibu tawala wa Wilaya hiyo Rachel Mhando amepiga marufuku mitumbwi na boti za wavuvi kuvusha abiria na kusema kuwa wanafanya kazi hiyo ni kinyume cha sheria wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria.
"Kunataviboti vinavusha watu nyakati za usiku na alfajiri ninyi TEMESA simamieni hili wasifanye hiyo kazi nihatari kwa maisha ya abiria " alisema.
Naye kaimu mtandaji Mkuu wa TEMESA Sylvester Simfukwe ameahidi kuyafanyiakazi maagizo yote yaliyotolewa na DC katika kuboresha huduma za Kivuko hicho.
Hivyo makala DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI
yaani makala yote DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/dc-kigamboni-atishia-kukifunga-kivuko.html
0 Response to "DC KIGAMBONI ATISHIA KUKIFUNGA KIVUKO CHA MAGOGONI"
Post a Comment