Loading...
title : KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI
link : KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI
KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI
WAZIRI WA Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema wamefanikiwa kukipindua kivuko cha MV.Nyerere na kukiweka sawa.
Kivuko hicho kilipinduka na kuzama katika ziwa Victoria Septemba 20 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 226 huku watu 41 wakipatikana wakiwa hai.
Akizungumza jioni hii kuhusu kivuko hicho Waziri Kamwelwe amesema hatimaye leo wamefanikiwa kukiweka sawa na kazi ambayo imebakia ni kukovuta ili kiwe mwaloni kwa ajili ya kuendelea na hatua iliyobakia."Tunashukuru makundi yote kwa namna ambavyo wamefanikisha kukiweka sawa kivuko hiki ambacho kilipinduka na kusababisha maafa ya Watanzania wenzetu.
"Zaidi ya watu 570 wameshiriki katika kufanikisha kivuko hicho tunakipindua baada ya kupinduka.Tunawashukuru wananchi wa Ukara kwa namna ambavyo wameshiriki katika kuokoa maisha ya watu 40,"amesema Waziri Kamwelwe.
Ameongeza kuwa kivuko hicho ambacho kimewekwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa TanzaniaVenance Mabeyo ataelezea hatua ambayo inafuata baada ya kukamilisha hatua ya kwanza.Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Venance Mabeyo amesema baada ya hatua ya kukisimamisha kivuko hicho kwa asilimia 85, kazi iliyobaki sasa ni kuondoa maji ambayo yamejaa ndani ya kivuko hicho.
" Kwa sasa tumefanikiwa kwa asilimia 85 kwani bado kuna hatua ambayo inafuata ya kuondoa maji,"amesema.Amefafanua baada ya kukipindua kivuko hicho na kisha kutoa maji watakivuta Mwaloni kwa ajili ya kuanza kufanyiwa matengenezo.Amesema pia watahakikisha wanasafisha eneo hilo ili kuangalia kama kuna chochote ambacho kimebakia na lengo ni kuacha eneo hilo likiwa salama."Tunataka wananchi Ukara wasiwe na hofu baada ya kukamilisha shughuli za kuondoa kivuko hicho kilipo na kukiweka Mwaloni," amesema Mabeyo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema msiba huo ulikuwa ni wa kitaifa licha ya kwamba limetokea mkoani Mwanza katika Wilaya ya Ukerewe katika eneo la Ukara.Amesema kuwa baada kikupindua kivuko hicho kwa sasa ni kuendelea kutoa maji yaliyomo.Amesema kuwa baada ya kutokea ajali hiyo Rais Dk.John Magufuli alikuwa akiwasiliana naye kwani alihakikisha anapata taarifa kwa kila kinachoendelea.
"Saa moja baada ya ajali hiyo kutokea Rais Magufuli alinipigia simu na kutoa maelekezo, pia nikapigiwa simu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa." Tunashukuru kwa ushirikiano ambao umeoneshwa baada ya kutokea ajali hii kwani Watanzania wote wameonesha kuguswa na ajali hii mbaya.Tuendelee kishikamana na ukweli tukio hili limetufundisha jambo kubwa,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.
Ametoa shukrani kwa makundi mbalimbali ambayo yameshiriki kikamilifu katika msiba huo ambapo pongezi hizo amezielekeza pia kwa vyombo vya habari kwa namna ambavyo wametoa taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea.
Hivyo makala KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI
yaani makala yote KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/kivuko-cha-mvnyerere-kilichoua-watu-226.html
0 Response to "KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI"
Post a Comment