Loading...
title : Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018
link : Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018
Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018
Na. VERO IGNATUS, ARUSHA
Ni septemba 29/2018 ni siku ua kuanza rasmi ligi daraja la kwanza msimu wa kwanza wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Mkoa huo ya Arusha United Wanautalii siku ya tarehe 29 wakati timu hiyo itakapomenyana na Rhino Rangers Fc ya Tabora.
Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Shekh Amri Abeid amesema anatarajia wana Arusha watajitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuishangilia timu hiyo ambayo kwa sasa inarudisha Mkoa huo katika ramani ya soka nchini ambayo imepotea kwa muda mrefu.
Jamillah amesema kikosi cha timu ya Arusha United wanautalii kimedhamiria kuingia ligi kuu mwakani kutokana na kuwa na kikosi imara chini ya kocha mkuu Felix Minziro ambae anahistoria safi katika soka nchini.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa timu ya Arusha United wana utalii Fikiri Elias amesema timu yake imejiandaa vyema kukabiliana na timu ya Rhino Rangers Fc kutoka Tabora na wauhakika na ushindi wa point tatu.
Kwa mara ya kwanza tangu ipate usajili timu ya Arusha United wana utalii itajitupa uwanjani rasmi kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka huu ikiwa katika safari yake ya kuelekea ligi kuu mwakani.
Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar
Hivyo makala Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018
yaani makala yote Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/arusha-united-wanautalii-kuivaa-rhino.html
0 Response to "Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018"
Post a Comment