Loading...
title : Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.
link : Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.
Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.
Na Mwashungi Tahir na Fatma Makame Maelezo 20-
9-2018.
Serikali inaendelea kuendeleza jitihada za kuondoa biashara
haramu ya ukahaba na mapenzi ya jinsia moja kwa Mkoa wa
Mjini Magharibi umefanikiwa kuwakamata wahusika 35 na
hatua za kisheria zinaendelea ikiwemo kupelekwa
Mahkamani.
Hayo ameyasema leo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa ,Serikali Za Mitaa na Idara Maalum Za SMZ Shamata
Shaame Khamis huko kwenye ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi wakati alipokuwa akijibu suala la Mheshimiwa
Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Paje aliyetaka kujua Je ni
watu wangapi waliokamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Alisema Malengo ya Operesheni hiyo imefanikiwa kwa kiasi
kukubwa ambapo imeweza kudhibitiwa kwa muda wa
kuanza na kumaliza burudani za muziki katika kumbi za
starehe, aidha imeweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa ya
matumizi ya shisha , udhalilishaji wa kijinsia na kusimamia
utaratibu wauzaji na matumizi ya video kwa muda wa saa za
kazi.
Pia Mkoa bado unaendelea na zoezi la kufanya operesheni ya
kushtukiza katika kumbi za starehe , vilabu vya pombe na
madanguro kwa lengo la kudhibiti kadhia hizo.
Aidha alisema zoezi linaendelea kutokana na malengo
tulojiwekea pamoja na kupata taratibu za sheria ikiwemo
jeshi la polisi kutoa elimu kwa jamii juu ya kutii sheria bila
ya kushirikishwa kutoa barua kwa maeneo yanayohusika
kwa biashara ya ukahaba ikiwemo Entebbe , Nyuki ,
Mwanyanya , Gofu na Mafunzo na kufungia madanguro
maeneo ya Miembeni pamoja na kuimarisha doria ya
kudhibiti madada na makaka poa.
Akiongeza suala la nyongeza Mh Jaku aliuliza kwa nini
harakati hizi za kudhibiti mambo haya mbona hazijagusa
watu wanaofanya vitendo vya jinsia moja.
Nae Naibu Waziri alimjibu kuwa wao wameamua kufanya
kwa wote wanaohusika na mambo ya ukahaba bila ya
ubaguzi wowote.
“Sisi tunawakamata wale wote wanaojihusisha na mambo ya
ukahaba na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bila
kubagua watu wa aina gani sheria inafata mkondo wake”.
Alisema Naibu Waziri huyo.
Nae Naibu Waziri wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali
Mmanga Mjengo Mjawiri akilijibu suala la Mh Ali Suleiman
Ali wa Jimbo la kijitoupele aliyetaka kujua Je Wizara ina
mpango gani wa kulinda usalama wa wanafunzi wa Skuli za
binafsi ambao wanajazwa sana katika magari.
Akijibu suala hilo Naibu huyo huko kwenye ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi alisema wizara bado inatambua kuwa
baadhi ya magari ya skuli binafsi yanayopakia wanafunzi
yanajaza kupita kiasi jambo ambalo linaweza kuhatarisha
usalama wa wanafunzi hao .
Alisema Wizara imekua ikilikemea suala hili katika mikutano
mbali mbali iliyofanyika na Skuli za binafsi au viongozi wa
umoja wa skuli hizo pia imewasilisha suala hili kwa kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na kutaka askari wa
usalama wa barabarani wawachukulie hatua za kisheria weye
magari wote watakaobainika wanakiuka taratibu za usalama
barabarani.
Mwisho.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.
Hivyo makala Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.
yaani makala yote Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/kutoka-baraza-la-wawakilishi-leo.html
0 Response to "Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo."
Post a Comment