Loading...
title : MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR
link : MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR
MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR
TAASISI ya Taaluma za kibenki Tanzania(TIOB) imefanya mahafali ya 18 ambapo wahitimu 157 wametunukiwa vyeti
Sherehe za mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pia wahitimu 22 wametunukiwa ngazi ya cheti, 133 wametunukiwa ngazi ya taaluma ya juu na 2 wametunukiwa vyeti vya kubobea katika masomo maalumu ya kibenki.
Pia katika sherehe za mahafali hayo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao walitunukiwa zawadi.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker amesema Sherehe ya mahafali zilitanguliwa na mkutano mkuu wa 20 wa mwaka kwaajili ya kutekeleza mpango wa 2018 wa TIOB pamoja na uteuzi wa Mkaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018.
Aidha Amesema kuwa taasisi ya TIOB imetoa wahitimu ambao wamebobea kwenye masuala ya benki.
Pia amewashauri wahitimu wote kufanya kazi kwa weledi kutokana na mafunzo waliyoyapata pia amewapongeza wahitimu wote kwa ushirikiano wao kwani wengine ni wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za benki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Benki TIOB Patrick Msusa amewapongeza Wahitimu wote.
Amewaomba watekeleze vyema majukumu yao katika kazi kwa misingi ya kibenki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akitoa hotuba yake katika mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker
Wahitimu wakiwa wamenyanya kofia tayari kwa kuvaa baada ya mgeni rasmi kutamka maneno ya kuwatunukia uhitimu wa masomo yao.
Wahitimu wakisikiliza neno kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker jijini Dar es Salaam wakati wa mahafari 18 ya mafunzo ya kibenki.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Hivyo makala MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR
yaani makala yote MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mahafali-ya-18-ya-tiob-yafanyika-dar.html
0 Response to "MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR"
Post a Comment