Loading...
title : MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO
link : MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO
MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO
Na Tiganya Vincent
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Serikali Mkoani Tabora kwa kufanya kazi zao kwa ushirikiano ambao umesaidia kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.
Alisema vyombo hivyo vinapaswa kuwa kitu kimoja jambo ambalo litawasaidia kubadilishana taarifa ili kufichua vikundi vya kihalifu kwa ajili ya kuhakikisha amani na salama miongoni mwa wananchi.
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Masanja alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi wa Serikali , Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipotembelea Ofisi ya Mkoa wa Tabora.
“Sio kila chombo kiende njia yake lazima kuwepo na umoja na mshikamano katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi” alisema.
Aliongeza kuwa na kila Wananchi analo jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi kwa kuchukua hatua za kutoa taarifa juu ya vikundi vya uhalifu katika maeneo yao ambazo zitaviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuzuia uhalifu.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkaribisha Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja ili aweze kuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja akizungumza na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya(kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya akuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora wakisikiliza Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja (hayupo katika picha) wakati alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya( wa tatu kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa mara baada ya kutembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO
yaani makala yote MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/meja-jenerali-masanja-amevipongeza.html
0 Response to "MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO"
Post a Comment