Loading...

MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

Loading...
MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA
link : MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

soma pia


MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA


NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE

NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amelitaka shirika la umeme (Tanesco) lizingatie kufikisha umeme katika taasisi za umma ikiwemo shule na zahanati ili ziondokane na changamoto hiyo. Aliyasema hayo ,kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe ,mkoani Pwani wakati alipokwenda kuwasha umeme kijijini hapo .

Subira alisema, kwanza shirika hilo lihakikishe linaipatia umma shule ya msingi Kisanga ili waondokane na adha hiyo.“Tanesco wakati wa kuunganisha umeme mhakikishe taasisi hizo ikiwemo zahanati,shule na ofisi za serikali zinapata umeme ili kurahisisha utoaji huduma kupitia miradi ya umeme vijijini (REA)” alisema.

Aidha Subira alieleza ,wizara ina malengo ya kuhakikisha umeme unawaka kila kijiji ambapo kwa sasa miradi iko mingi lengo likiwa ni kufanikisha suala hilo.“Pia wananchi wanapaswa kutumia miradi hiyo kwani itakapokwisha bei haitakuwa hii ya 27,000 itaongezeka hivyo wachangamkie fursa hiyo,” alisisitiza Subira. Diwani wa kata ya Kisanga, Pili Chambuhi alisema,kijiji hicho kupata umeme ni mkombozi kwao kwani utasaidia kufanya shughuli ndogondogo za ujasiriamali. Alielezea hadi sasa jumla ya nyumba 60 zimeunganishiwa umeme.Pili, alisema kuwa shirika hilo linapaswa kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo ya ndani ndani na si maeneo ya barabarani peke yake.

Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akionyesha ishara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.


Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani. 


Hivyo makala MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

yaani makala yote MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mgalu-awasha-umeme-kijiji-cha-kisanga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA"

Post a Comment

Loading...