Loading...
title :
link :
Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa was Dar es Salaam Paul Makonda amekagua miradi ya Ujenzi wa barabara Wilaya ya Kigamboni na kutoa maelekezo kwa Tanrods kuweka alama kwenye maeneo yote yaliyokatwa au waliochimba ili kuweza kusaidia kupunguza adha za jali hasa kwa waendesha Bodaboda.
Rc Makonda ameyasema hayo Leo ambapo amefanya Ziara katika Manispaa hiyo, na kukagua kazi inayofanywa na Tanrods Pamoja na Tarura na kuwapongeza kwa kazi wanayoifanya ndani ya Manispaa hiyo.
Amesema watahakikisha katika barabara zinazojengwa katika Daraja la Nyerere, Kigamboni wanaweka miundo mbinu mizuri ili kuwafanya wananchi wanaozungukwa na barabara hizo kunufaika na mradi huo was barabara.
"Katika barabara sita zianzojengwa katika Daraja la Kigamboni nimemwambia Mkuu wa Wilaya kuhakikisha tunajenga miundombinu rafiki kwa wananchi wanaozungukwa hapa,ikiwemo kujenga Stand, Kuhakikisha Kuna sehemu ya kivuko Cha waenda kwa miguu,na mferji wa mita 400 ambao umeshatengenezwa na kuhakikisha maji yanapita"Amesema Makonda.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapohitajika hasa wanapoitwa katika mikutano ili kushiriki katika kutatua kero zinazokabili Wilaya hiyo.
Amesema katika halmashauri ya Kigamboni kunajengwa shoorom ya kisasa ya Afrika Mashariki, hivyo wameamua kutatua kero za miundombinu ikiwemo barabara umeme Pamoja na maji ili kusaidia kuwepo kwa Viwanda vitakavyoongeza pato la Manispaa hiyo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara. Amemshukuru Rc Makonda kwa kufanya ziara Katika halmashauri yake, na kutoa maelekezo katika miradi ya kimkakati
Hasa kwenye miradi ya barabara.
Amesema katika kutekeleza Sera ya serikali ya Awamu ya tano, kwamba Kila Wilaya iwe na mapato ya ndani wameamua kutengeneza miundombinu ili kurahisisha upatikanaji wa mapato na kuweza kufikia malengo ya serikali ya Awamu ya tano.
Mradio huo utakuwa na barabara sita itakayounganisha barabara ya kuelekea Kibada na barabara ya kuelekea feri ambapo hadi kufikia Oktobar 31 mwaka huu,mradi huo utakuwa umekamilika utakao changia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato kwenye Wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mwambawahabari-mkuu-wa-mkoa-was-dar-es.html
0 Response to " "
Post a Comment