Loading...
title : NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA
link : NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA
NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha taarifa mbalimbali za hospitali wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kulia kwake ni katibu wa afya wa hospitali hiyo Mwanaisha Hassan.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray inafanya kazi ndani ya siku 14.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali hiyo leo jijini Dodoma.
"Ifikapo Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya" alisisitiza Dkt. Ndugulile
Aidha,Dkt. Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini hapo.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe wa watendaji wa Hospitali hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa kwa vitendo.
Wakati huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo takribani ya kutosha miezi sita kwenye stoo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikagua maboksi ya sindano katika stoo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa waliokua wanasubiri huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali hiyo.
Hivyo makala NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA
yaani makala yote NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/ndugulile-atoa-siku-14-kukamilishwa-kwa.html
0 Response to "NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA"
Post a Comment