Loading...

NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

Loading...
NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA
link : NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

soma pia


NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

BENKI ya NMB Plc imesema itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma.

Mpango huo ulielezwa jana na Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa mazungumzo mafupi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma.

Mponzi alisema kwa sasa NMB inawasaidia zaidi ya wakulima wadogo wadogo milioni moja nchi nzima, na kwamba benki itaendelea kutenga fedha za kutosha ili kusaidia wakulima wengi zaidi. “Kwa sasa, NMB imetenga zaidi ya shilingi billioni 500 kwa ajili ya kusaidia wakulima hapa nchini lengo likiwa kusaidia jitihada za serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Serikali inapeleka nguvu zake katika kukuza kilimo cha zao la mchikichi mkoani Kigoma, na hivyo akaitaka benki ya NMB kuisaidia Serikali katika kufanikisha azma hiyo kwa kuwasaidia wakulima wa michikichi mkoani humo.

“Tumekuwa tukiwashawishi wakulima mkoani Kigoma kujikita katika kilimo cha michikichi lakini kwa bahati mbaya wakulima wengi hawana mitaji ya kulima michikichi kwa wingi. Nitafurahi kama benki yenu kupitia mikakati yake itawawezesha wakulima wa michikichi,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu ameomba kukutana na uongozi wa benki ya NMB mapema wiki ijayo mkoani Kigoma ili kwa pamoja waweze kupanga mkakati kazi wa kuwasaidia wakulima mkoani humo kulima michikichi kwa ufanisi na wingi zaidi. 

Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi (kulia) akitoa maelezo ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo jana Jijini Dodoma kwenye monyesho ya Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT). Benki ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufadhili mkutano huo, ikiwa ni kwa mwaka wa sita mfululizo sasa. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi pamoja na Meneja Mwandamizi wa Biashara za Kilimo wa NMB -Isaac Masusu.
Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wakati wa mkutano mkuu wa 34 wa jumuiya hiyo unaoendelea jijini Dodoma.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>


Hivyo makala NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

yaani makala yote NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/nmb-sasa-kusaidia-kilimo-cha-michikichi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA"

Post a Comment

Loading...