Loading...
title : PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU
link : PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU
PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Manga uliopo Wilaya ya Mpanda Mjini, mkoani Katavi achunguzwe na TAKUKURU kutokana na kutumia mabomba yasiyokidhi viwango.
Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha majumuisho na uongozi wa mkoa mara baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Katavi.
Mradi huo wa Manga wenye thamani ya Shilingi milioni 575 unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingia mjini Mpanda (MUWASA) na kutekelezwa na mkandarasi anayejulikana kama Nyalinga Investment Co. Ltd, uligundulika kuwa una kasoro ya mabomba mara baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mji wa Mpanda (MUWASA), Mhandisi Zacharia Nyanda kubaini ubovu wa mabomba hayo na kuyapeleka Shirika la Ubora wa Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya vipimo na kuonekana hayakidhi viwango.
Amesema kuwa ripoti hiyo ya TBS imeonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya vipimo vya mabomba yaliyotumika na vipimo vinavyoonekana kwenye mkataba, hivyo kuthibitisha udanganyifu wa mkandarasi huyo na kumpongeza Mhandisi Nyanda kwa kugundua mapungufu hayo.
‘‘Nampa pongezi Mkurugenzi wa MUWASA kwa kugundua jambo hili; mabomba haya hayaonyeshi hata yametengenezwa wapi, achilia mbali kutofautiana kwa vipimo na vile vilivyo kwenye mkataba. Huu ni udanganyifu wa hali ya juu, ambao nimekuwa nikiusema kuhusu wakandarasi wababaishaji na sitafumbia macho wakandarasi wa aina hii’’, amesema Profesa Mbarawa.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwaonyesha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mpanda Mjini ushahidi wa ripoti ya TBS juu ya mabomba mabovu yaliyotumika kwenye mradi wa Manga, mkoani Katavi. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi, Mhandisi Edward Mulumba (kushoto) na mbele yao ni Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji mjini Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na wakandarasi eneo la mradi Nzega.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi, Mhandisi Edward Mulumba (kushoto) na mbele yao ni Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji mjini Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na wakandarasi eneo la mradi Nzega.
Hivyo makala PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU
yaani makala yote PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/profesa-mbarawa-aagiza-mkandarasi.html
0 Response to "PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU"
Post a Comment