Loading...
title : THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama
link : THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama
THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BARAZA la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Juu (THU) limesema kuwa litaendelea kuwa na busara katika kufatilia madai yao kwa kufuata taratibu za Kiutumishi.
Baraza hilo lilikutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya stahiki zao katika vyuo vya umma nchini.
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha wafanyakazi Taasisi ya elimu ya juu (THTU) Paul Liosure akizungumza katika baraza hilo amesema kuwa serikali kuna vitu imefanya vizuri lakini vingine bado vinavyohusiana na madai hivyo busara lazima itumike.
Amesema kuwa kuna Mamlaka za serikali ambazo zipo kwa ajili yao ambazo zinatakiwa kuzifikia katika kupata ufumbuzi.
Liosure amesema kikao cha baraza ni cha dharula kwa wanachama kuwa na dukuduku kuhusiana madai yao katika utumishi wa umma.
Aidha liosure ameeleza kwakina dhumuni la kikao hicho ni kutoa muelekeo juu ya maslahi ya wafanyakazi kwani wengi wao wamekua wakilalamikia masilahi ya malimbikizo ya mishahara ikiwa baadhi yao walishalipwa katika awamu zilizopita.
Liosure amesema madai hayo yalishapelekwa kwa sehemu husika na swala hilo litapelekwa pamoja na wataandaa walaka wa matatizo ya watumishi ili waweze kushughulikiwa.
Mwenyekiti huyo amefafanua kuhusu sheria zilizojadiliwa ni pamoja na sheria ya bodi ya mikopo na wameona ipo haja ya kupendekeza sheria na kanuni hizo kwa serikali ili kuboresha kanuni na sheria hizo kwa lengo la kuleta nafuu kwa watumishi.
Mwenyekiti wa chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu (THU) Liosure akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Chama hicho kuhusiana na madai mbalimbali ya masilahi ya Wafanyakazi wa taasisi ya Elimu ya Juu.
Viongozi wa THU wakiwasikiliza wajumbe wa baraza hawapo pichani
Picha mbalimbali wajumbe wa baraza hilo.
Hivyo makala THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama
yaani makala yote THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/thu-yakutana-kujadili-masilahi-ya.html
0 Response to "THU yakutana kujadili masilahi ya wanachama"
Post a Comment