Loading...
title : WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO
link : WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO
WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO
Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi nchini wameaswa kutoa wataalamu wa maendeleo ya Jamii wenye viwango vya juu ili kuendana na ushindani uliopo na katika kufikiamuchumi wa kati na wa viwanda.
Hayo yamesemwa leo Mjini Singida na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni na utakaoanza kutumika kwa mwaka wamasomo 2018/2019 mpaka mwaka 2022/2023.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bw. Golwike amewapongeza wakuu wa vyuo na wakufunzi hao kwa kazi nzuri wanaoendelea kufanya katika kutoa wataalamu wenye viwango katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.
Ameongeza kuwa wakufunzi hao wanatakiwa kuongeza nguvu katika kutengeneza wataalamu wengi wenye viwango zaidi ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na ushindani katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.
“Tutengeneza wataalamu wenye viwango ili tuendane na mabadiliko hasa kuelekea uchumi wa viwanda” alisisitiza Bw. Golwike
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi upande wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akielezea lengo na umuhimu wa mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bw. Paschal Mahinyila akitoa salamu za Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo wa wakuu kwa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Mwakilishi kutoka NACTE Bw. Gidion Karuguru akitoa muongozo wa matumizi ya Mtaaka Mpya kwa Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Wakuu wa Vyuo na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia mafunzo ya Mtaala mpya kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi nchini uliopitishwa na NACTE hivi karibuni utakaoanza kutumika kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Picha zote na Kitengo cha Mawasilino WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO
yaani makala yote WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/wakufunzi-vyuo-vya-maendeleo-ya-jamii.html
0 Response to "WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO"
Post a Comment