Loading...
title : WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI.
link : WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI.
WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI.
Watumiaji wa simu nchini Kenya huenda wakatozwa ada zaidi katika ununuzi wa muda wa maongezi na huduma ya mtandao.Hii ni baada ya serikali kutangaza mpango wa kuongeza kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kutoka 10% hadi 15%.
Nyongeza hiyo imejumuishwa katika pendekezo la rais Uhuru Kenyatta kwa bunge kufuatia tamko lake la wiki iliyopita.
Pendekezo la tozo hilo jipya la kodi likiidhinishwa na bunge litatekelezwa wakati ambapo watumiaji wa simu wanakabiliwa na gharama ya ongezeko la ada ya huduma za kutuma pesa.
Miongoni mwa aliyopendekeza rais Uhuru kando
Kuongeza kodi ya VAT kwa watumiajiwa simu kutoka 10% hadi 15%Rais Uhuru ametangaza kupunguza kodi ya mafuta kutoka 16% hadi 8%.
Kupunguza gharama za mapokezi , burudani, mafunzo na mikutano, na usafiri katika nchi za nje.Kuongeza fedha katika idara za utekelezaji wa sheria kuweza kukusanya mapato zaidi kupitia mahakama ya nchini.
Rais Kenyatta amesema kuwa bado kuna pengo katika bajeti ya serikali na ndio sababu amependekeza hatua hizo za kufunga mkaja au kubana matumizi katika idara zote za serikali
Mapendekezo hayo, hata hivyo yanatarajiwa kujadiliwa bungeni siku ya Alhamisi.
Hivyo makala WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI.
yaani makala yote WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/watumiaji-wa-simu-kutozwa-kodi.html
0 Response to "WATUMIAJI WA SIMU 'KUTOZWA' KODI."
Post a Comment