Loading...

WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI

Loading...
WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI
link : WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI

soma pia


WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wachimbaji wadogo wa madini waende Benki wakakope mitaji kwa sababu wana uhakika wa kudhaminiwa na Benki Kuu.

“Msihofu kukopa, kukopa ni jambo la kawaida sana. Nenda mkakope ili mpate mitaji ya kununua mitambo ya kuchenjua dhahabu na madini mengine,” amesema.

Ametoa wito leo (Jumapili, Septemba 30, 2018) wakati akifunga maonesho ya mkoa wa Geita ya dhahabu, madini, teknolojia ya madni na uwekezaji yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita. Maonesho hayo yalianza Septemba 24, mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema, wakati akikagua mabanda ya maonesho kwenye viwanja hivyo, ameelezwa kwamba gharama ya mtambo unaohitajika kwa wachimbaji wa kati inafikia sh. milioni 10. “Naomba niwaeleze wanaGeita kwamba mnakopesheka, nendeni mkaombe mikopo ili mnunue mitambo ya kuchenjua dhahabu,” amesisitiza.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaeleza wana-Geita kwamba siri kubwa ya kufanikiwa kupata mikopo ni kwa wao kuunganisha nguvu kwa kujiunga kwenye vikundi ili wawe na malighafi ya kutosha mitambo hiyo.

“Wakuu wa wilaya za Mkoa huu simamieni zoezi hili kwa sababu wilaya zenu zote zinachimba madini. Simamieni uundaji wa vikundi na mwende mkawasemee benki pale wanapokwama.”

Akielezea kuhusu makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya dhahabu kwenye mkoa huo, Waziri Mkuu amesema tangu Aprili mwaka huu, mapato yanayotokana na madini yameongezeka kutoka sh. milioni 400 na kufikia sh. milioni 850 Agosti, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wazazi wawapeleke watoto wao kwenye vyuo vya ufundi vya VETA ili wakajifunze taaluma ya uchongaji wa madini na vito kama eneo jipya la ajira nchini.
 Mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo cha VETA Moshi, Careen Vedasto akiendesha kifaa cha kuchimbia madini kilichobuniwa na wanafunzi na walimu wa chuo hicho mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuuliza maswali mwanafunzi wa VETA Moshi, Jesca Jonathan (mwenye rasta), kuhusu utaalamu wa kuchonga vito na madini alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Wa pili kulia ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kifungashio cha kopo la kahawa aina ya AMIMZA alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kulia ni Afisa mauzo wa TANICA PLC, Revina Peter akitoa maelezo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya mtambo wa kuchenjua madini unaoweza kumilikiwa na wachimbaji wa kati alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Anayetoa maelezo ni Katibu Msaidizi wa UMUMAGE, John Ngenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI

yaani makala yote WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/waziri-mkuu-ataka-wachimbaji-wadogo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI"

Post a Comment

Loading...