Loading...
title : ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050
link : ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050
ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050
Na Mwandishi Wetu -Arusha
Tanzania inakadiliwa itakuwa na wazee 11% ya watu wote nchini ifikapo mwaka 2050, kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka kwa kasi kutokana na kuendelea kuboreka kwa huduma za Afya hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Edward Mung’ong’o wakati akiwasilisha mada kwenye kongomano lililofanyika leo Jijini Arusha kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee, amesema kuwa Mwaka 2002 idadi ya Wazee ilikuwa milioni 1.4, ikiwa ni sawa na 4% ya watu wote yaani Milioni 33.5.
Aidha Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa kwa sasa idadi ya Wazee hapa nchini inakisiwa kuwa milioni 3 sawa na 5.6% ya watu wote ambao kwa takwimu za sasa Tanzania ina Watu milioni 55.
Akizungumzia mafanikio ya serikali katika kuboresha huduma za Afya kwa Wazee Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la HelpAge International imepitia na kuboresha Mtaala wa kufundishia Wauguzi ngazi ya kata ili wapate mafunzo yatakayowawezesha kuhudumia Wazee kwa ufanisi.
Aidha Dkt. Mung’ong,o aliongeza kuwa kwa kushirikiana na HelpAge International pia serikali imeandaa Mwongozo kwa ajili ya watoa huduma wa kuwaelekeza jinsi ya kutibu magonjwa ya kawaida yanayowasibu Wazee.
Wakati huo huo Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisema Wazee watatumia fursa hiyo kujadiliana juu ya utekelezaji wa Sera na Miongozo ya kuboresha hali na Maisha ya Wazee nchini kwa kuzingatia utambuzi wa wazee katika Halmashauri, upatikanaji wa huduma za Afya kwa wazee na ushirikishwaji wa wazee.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi akielezea lengo la kongamano kwa wazee waliohudhuria kongamano la wazee kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika Jijini Arusha Oktoba Mosi.
Mwenyekiti wa Kongomano la Wazee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania Mzee Sebastian Bulegi akiongoza Wazee walioshiriki katika kongomano la wazee kwa lengo la kujadili changamoto wanazokabiliana nazo wazee nchini wakati wa kongamano la wazee kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika Jijini Arusha Oktoba Mosi.
Mratibu wa huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Edward Mung’ong’o akiwasilisha mada wakati wa kongomano kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo Jijini Arusha.
Kamishana wa Polisi akieleze kuhusu hali ya mauaji ya wazee nchini na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo katika kupambana na vitebdo vya ukatili kwa wazee wakati wa kongomano kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo Jijini Arusha.
Wazee walioshiriki Kongamano la Wazee wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa katika Kongamano hilo ikiwa ni moja ya shighuli zinazofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika Jiji la Arusha Oktoba Mosi. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050
yaani makala yote ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/asilimia-11-ya-watanzania-kuwa-wazee.html
0 Response to "ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050"
Post a Comment