Loading...

ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

Loading...
ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO
link : ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

soma pia


ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA 

DAKTARI Bingwa bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) ya jijini Mwanza Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) anayedaiwa kujifanya daktari atafikisha mahakamani muda wowote.

Samweli aliangukia mikononi mwa jeshi la polisi jijini Mwanza akituhumiwa kujifanya daktari bandia ambapo alikamatwa Oktoba 3,mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni katika Hospitali ya BMC akiwa katika chumba cha upasuaji. Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wagonjwa waliyotaoa kwa uongozi wa hospitali hiyo pamoja na jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna akizungumza na waandihi wa habari jana alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na kunaswa akiwa kwenye chumba cha upasuaji atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema kabla ya kutiwa mbaroni mtuhumiwa huyo alikuwa akijifanya ni daktari bingwa na alifanikiwa kuwatapeli baadhi ya wagonjwa wanaotaka kupata huduma za upasuaji na matibabu kwa njia za mkato kwa kuwatoza kati ya sh. 100,000 na 200,000 ili awapangie tarehe za karibu wapate huduma hizo.

Kwa mujibu wa ACP Shanna mtuhumiwa huyo tapeli ni mkazi wa Mtaa wa Pasiansi katika Manispaa ya Ilemela ingawa awali alipohojiwa kwenye Hospitali ya BMC alidai ni mkazi wa wilayani Magu.

“Jeshi la polisi tulipokea malalamiko ya wagonjwa kutapeliwa na kuibiwa mara kwa mara wodini na hivyo tuliwaelekeza wayafikishwe kwa uongozi wa hospitali.Tuliweka mtego tukishirikiana na na uogozi wa hospitali hiyo ya rufaa BMC tukafanikiwa kumnasa akiwa kwenye chumba cha upasuaji akiwa amevalia sare zinazovaliwa na madaktari wakiwa theater,” alisema ACP Shanna.
Daktari bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) akiwa kwenye kituo cha Polisi Kati Nyamagana, kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Jonathan Shanna wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa daktari huyo bandia. 



Hivyo makala ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

yaani makala yote ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/abambwa-kwa-kujifanya-dk-bingwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO"

Post a Comment

Loading...