Loading...
title : BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA
link : BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA
BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA
Na Stella Kalinga, Simiyu.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amesema angependa kuona katika kipindi chake atakachokuwepo hapa nchini akiiwakilisha nchi ya Kenya ushirikiano wa kiabishara katika Kenya na Tanzania na unaimarika na takwimu za biashara, viwanda na uwekezaji kati ya nchi hizo zikiongezeka mara dufu.
Balozi Kazungu ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery LTD), kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Oktoba 05, 2018 katika ziara yake mkoani Simiyu.
Balozi Kazungu amesema ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hususani katika viwanda, kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea kuimarika zaidi utachangia kuongeza ajira, kuwatoa wananchi katika umaskini pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo pia.
“Baada ya miaka minne kazi yangu kama ikiisha hapa, naomba nione takwimu za viwanda, biashara, uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya zinaongezeka mara dufu, nafasi za kazi kwa watu wetu zinapatikana na watu wetu wanaondokana na umasikini; kukua kwa Tanzania kuwe ndiyo kukua kwa Kenya hilo ndiyo ombi letu” alisema Mhe. Balozi Kazungu.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kushoto) akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani humo, wakati ziara ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa nne kulia) kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa tatu kushoto) akiangalia pamba iliyochambuliwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018 (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na (wa pili kushoto) Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) wakiwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini kenya(kulia), akimuongoza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu, kuelekea katika moja ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA
yaani makala yote BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/balozi-kazungu-ningependa-nione-takwimu.html
0 Response to "BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA"
Post a Comment