Loading...
title : BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII.
link : BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII.
BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ng’wilabuzu Ludigija ,akizungumza katika Baraza la madiwani aliye upande wa kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Maabadi Hoja .
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imewataka wakazi wanaoisha katika eneo la mabonde hatarishi kuchukua tahadhali ikiwemo kuhama kabla kipindi cha mvua kuanza ili wasije kupatwa na maafa.
Tahadhali hiyo imetolewa na mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Maabadi Hoja, wakati akijibu maswali katika Baraza la madiwani katika kikao cha robo ya kwanza ya Mwaka , ambapo amesema kuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo atapita na timu ya watendaji wake kuyaainisha maeneo hayo na kuona yanausalama gani.
"Wito wangu ni kwamba kila anayejifahamu kuwa anaishi katika maeneo hatarishi anatakiwa aondoke kwa hiali yake kabla ya kupatwa na Maafa" alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo Ng'wilabuzu Ludigija amesema Manispaa inafanya jitihada za kukamilisha ujenzi wa shule mbili za sekondari ikiwezekana ziweze kupandishwa hadhi ziwe na kidato cha sita ambapo shule moja iko Kigamboni na nyingine katika eneo lakata ya Somangila ambayo tayari miundombinu yake yote imekamilika kujengwa kilichosalia ni bwalotu.
Amesema Halmashauri hiyo ilitegemea pesa kutoka serikali kuu kupitia fedha za maendeleo (CDG) na hawakuwahi kuingiza katika bajeti ya ndani na changamoto iliyo sasa ni namna ya kupata fedha, lakini wameamua kuchukua fedha kutoka vyanzo vingine ili kukamilisha ujenzi huo.
Kwa upande wa sekta ya Afya Ng'wilabuzu amesema Halmashauri imepokea shilingi milioni 500 kutoka ofisi ya Rais Tawala zamikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kwaajili ya ujenzi wa Hospitali eneo la Nafco, na wizara ya fedha imeadhimisha kutoa shilingi billion 1 kwaajili ya ujenzi huo, pia kupitia vyanzo vya ndani wanatarajia kukamilisha ujenzi wa Kituocha afya Kimbiji.
Pamoja na hayo ameshukuru serikali kuu kwa kuijali Kigamboni kuendelea kutoa fedha za miradi na kusema kuwa wamepeleka maombi maalumu ili kupatiwa fedha za kumalizia ujenzi wa ofisi za Manispaa kwa kuwa walipopanga kwa muda huu hapatoshi wanaishi kwa kubanana jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa watumishi katika kutekeleza majukumu yao.
"Tumeomba watupatie fedha ukifika katika katika ofisi yetu utaonana tunafanya Kazi katika mazingira magumu watumishi wanafanya Kazi hadi Koridoni Idara zingine zimekosa ofisi, tunaamini wakitupatia tutakamisha angalau ghorofa moja tuhamie ifikakapo mwezi February mwakani" alisema.
Naye Mhandisi wa Manispaa hiyo Pius Mutechura, kwa niabaya Mkurugenzi, akijibu swali la Diwani wa kata ya Kigamboni Dotto Msawa kuhusu kufanya ukarabati wa maeneo korofi yanayo jaamaji amesema maeneo hayo yatafanyiwa kazi ilikuyaweka katika hali nzuri na kwamba wanaendelea na mazungumzo na bandari ya Dar es salaam ili waweze kupewa eneo kwaajili ya stendi kwani iliyopo imekuwa ndogo kutokana na ongezeko la watu naMagari.
Hivyo makala BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII.
yaani makala yote BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/baraza-la-madiwani-kigambo0ni-laweka.html
0 Response to "BARAZA LA MADIWANI KIGAMBO0NI LAWEKA MIKAKATI MIZITO KUKAMILISHA MIRADI HII."
Post a Comment