Loading...
title : BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY
link : BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY
BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii.
UONGOZI wa Shule ya Msingi Misray iliyopo wilayani Kondoa wameishukurua benki ya TPB kwa kuwasaidia kuwajengea vyumba viwili vya madarasa,ofisi za walimu pamoja na samani zake.
Umesema msaada huo sasa utaondoa changamoto kubwa ambayo walimu na wanafunzi wa shuleni hapo walikuwa wanaupata ikiwemo ya kukatisha masomo pindi mvua inaponyesha.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misray Veronica Gabriel ametoa shukrani hizo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dk.Edmund Mndolwa.
Ambapo makabidhiano ya msaada huo yalifanyika shuleni hapo na mgeni rasmi alikuwa Dk.Kijaji ambaye ndiye aliyekabidhi kwa uongozi wa shule hiyo.Mwalimu Gabriel amesema kuwa wanatoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo na kuahidi msaada huo wa majengo watautunza pamoja na samani zote ambazo zimetolewa."Napenda kuwahakikishia uongozi wa Benki ya TPB kuwa huu msaada umesaidia kutatua tatizo la uhaba wa majengo duni yaliyooezekwa kwa nyasi na ilitulazimu kukatisha masomo pindi mvua inaponyesha.
" Kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa sana .Tunatoa rai kwa taasisi nyingine kutoa misaada kama hii kwa ajili ya kuondoa changamoto zilizopo,"amesema.Kwa uoande wake Dk.Mndolwa amesema wao kama taasisi ya fedha inayohudumia jamii wameguswa na matatizo hayo na ndio maana walipopokea naombi kutoka kwa uongozi wa shule hiyo wakaona ni vema wakasaidia.
"Tumetoa msaada huu baada ya kushuhudia mazingira magumu ambayo watoto hawa walikuwa wanakabiliana nayo kutokana na kukosa majengo ya madara." Hawa watoto wetu sote na ni jukumu letu kama wazazi kuona umuhimu wa jambo hili la kuwasaidia kwani hawa watakuwa viongozi wetu wa baadae.Ujenzi umegharimu Sh.Milioni 63 ,"amesema Dk.Mndolwa.
Kutokana na msaada huo shule hiyo imefanikiwa kutatua changamoto ya tatizo la madarasa,ofisi ya walimu na samani zake baada ya benki hiyo kusaidia.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa jengo la darasa katika Shule ya Msingi Misray wilayani Kondoa.Majengo hayo yamejengwa na Benki ya TPB

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB Dk.Edmund Mndolwa wa kwanza kulia pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji anayefuata wakiwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali na walimu wakati wa kukabidhiwa kwa majengo mawili ya madarasa, ofisi na samani kwa shule ya msingi Misray.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akiwa pamoja na viongozi wa benki ya TPB na wanafunzi wa Shule ya Msingi Misray wilayani Kondoa baada ya kukabidhiwa msaada wa majengo mawili ya madarasa,ofisi za walimu na samani zake
Hivyo makala BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY
yaani makala yote BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/benki-ya-tpb-yasaidia-kutatua.html
0 Response to "BENKI YA TPB YASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADARASA,OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MISRAY"
Post a Comment