Loading...
title : WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA .
link : WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA .
WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA .
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Wavuvi ,wafanyabiashara na Mama Lishe wa Soko la Feri wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli kwa mchango wao waliowapatia kwaajili ya kujenga ofis na kuendeleza biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa bodi ya soko feri Henry Sato Massaba, kwa niabaya wavuvi hao ametoa shukrani hizo na kusema kuwa Rais Magufuli alikuwa katika matembezi yake akifanya mazoezi juzi alizungumza na wavuvi na kuwaahidi kuwapa Pesa shilingi million 20 huku mkewe akiahidi kutoa shilingi Milion 5 kwa mamakishe wa zone namba 8 na kusema kuwa ahadi hiyo ameitimiza na kwa kutoa pesa hizo.Mtakumbuka Rais alikuja mwaka 9 December 2015 baada ya kuapishwa alifanya usafi katika zone hiyo hiyo na wadau wetu walimlilia kilio na juzi alitoa hizo pesa kwa vikundi vyetu vya (UWAWAKI) na Mkewe naye alitoa kwaajili ya mamalishe tunamshukuru sana kwa mchango huo na upendo aliotuonesha , na kusimamia mabadilko katika soke hili ambalo ni lakimataifa na tunapigania kilasiku liwe na hadhi yakimataifa” alisema
Kwaupande wake mwenyekiti wa zone namba tatu ,Omary Mwinyi makungu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya wadau ,amesema kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kwani wamehangaika muda mrefu na wanamshukuru kwa kutambua mchango wao na kusema kuwa wao ndiyo walipambana hadi kuongezeka kwa mapato ya soko hilo kwa kupiga vita watu waliokuwa wakijinufaisha wao waowenyewe ambapo zamani makusanyo yalikuwa shilingi million 18 na sasa million 100.
‘’Hilisoko baada ya kupambana tuka pata bodi tumeanza kuyaona mafanikio na tuna mshukuru waziri Jafo , soko halikuwa hata na Akaunti akaagiza ikafunguliwa na sasa hataukarabati wa soko na ujenzi wa miundo mbinu inafanyika ‘’ alisema .
Amesema soko la Feri ni moja ya masoko machache mazuri barani Afrika nila pili kwa ukubwa ukitoka lilie la Senegal lakini wenzetu wanaendesha vizuri soko lao na mapato yake yanazunguka hapo hapo lakini sisi haikuwa hivyo baada ya sisi kupigania tuka itwa wezi ,ila nashukuru wametuelewa sasa wezi na wadokozi hawapo tena .
Aidha ameomba kupatiwa mafunzo kwa kikundi cha ulinzi shirikishi maana kimetumika muda mrefu na kimesaidia sana na kusema kuwa pamoja na kwamba kuna ulinzi kutoka SUMA JKT lakini wasi sahaulike.
Naye Ashura Seif Nanjonga ,wa kikundi cha Baba na Mamalishe UBAMALE akizungumza kwa niaba ya Mama na Baba lishe waliopewa shilingi million tano amemshukuru Mama Janeth Magufuli na mumewe kwa moyo wao walio unesha kwa kuwapenda wanyonge .
“ Pesa hizo tumeziweka Bank wakati zinakuja kiongozi waetu hakuwepo ila sasa asharudi na pesa hiyo tutaanza kuitumia kama tulivyo kuwa tumepanga hapo awali , katika kikundi chetu tuko watu 50 na hatuna hata mabanda tuko juani hizi pesa zitatusaidia angalau hata kwa kuweka kivuli hata miamvuli ya kujikinga na jua na mvua’’alisema
Hivyo makala WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA .
yaani makala yote WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wavuvi-na-mamalishe-wamshukuru-rais-dkt.html
0 Response to "WAVUVI NA MAMALISHE WAMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA MSAADA ALIOWAPATIA ."
Post a Comment