Loading...
title : DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI
link : DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI
DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko leo amefungua semina ya wadau wa uhifadhi, udhibiti na usimamizi wa kemikali hatarishi hapa nchini.
Akizungumza na wadau hao jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa semina hiyo inatawakumbusha na kuwajenge uwezo wadau wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003.
Pia amewaasa kutunza na kusimamia kwa usalama kemikali hatarishi ambazo zinaweza kuleta madhara kwa binadamu na mazingira ndani ya bandari.
“Nawasihi msikilize kwa makini mafunzo haya ili utakapoanza kwenda kwenye ukaguzi uende kutekeleza matakwa ya Sheria na kanuni zake na sio kwa hiari yako. Kuna vifungu vya sheria ambavyo vinakuhusu kama mkaguzi na utatakiwa kuwajibika pale utakapoenda kinyume chake. Sheria inaainisha wajibu na majukumu ya mkaguzi na pia mkaguliwa, hivyo mnapaswa kuwa makini na kuelewa majukumu na wajibu wenu". amesema Dkt. Mafumiko
Mkemia Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali, Daniel Ndiyo akizungumza wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Baadhi wadau wakiwa katika mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya wadau wa uhifadhi usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.
Hivyo makala DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI
yaani makala yote DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/dkt-mafumiko-amewaasa-wadau-wa-kemikali.html
0 Response to "DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI"
Post a Comment