Loading...

FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

Loading...
FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA
link : FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

soma pia


FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Fainali za mashindano ya vilabu vya kodi zilizoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zimefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Shule za Sekondari zilizoibuka na ushindi na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano hayo.

Fainali hizo zilizofunguliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilifanyika jana katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Shule ya Sekondari St. Joseph iliibuka mshindi wa kwanza kati ya shule 28 za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuzawadiwa runinga, kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti.

Shule ya Sekondari Tumbi imeshika nafasi ya pili ambayo ilijinyakulia kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Dar es Salaam ambayo ilipata ngao, kompyuta ya mezani, saa ya ukutani na cheti.

Kwa upande wa uwasilishaji mada zinazohusu masuala ya kodi, Shule ya Sekondari Zanaki iliongoza na kuzawadiwa kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali na cheti ikifuatiwa na Kerege ambayo ilijibebea printa, saa ya ukutani na cheti huku Shule ya Sekondari Misitu ikishika nafasi ya tatu na kuondoka na kompyuta ya mezani, ngao, na cheti.

Kwenye kipengele cha Ukusanyaji wa Risiti za Kielektroniki za EFD, walioibuka washindi ni Shule ya Sekondari Gerezani ambayo ilizawadiwa runinga, fedha taslimu shilingi 1,000,000, cheti na medali. Mshindi wa pili ni St. Joseph iliyojitwalia ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 750,000 ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Benjamini iliyopata ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 500,000.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwakabidhi zawadi wanafunzi wa St. Joseph wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye umri wa mika 12 wa Shule ya Sekondari Mbezi Inn, Charles Denis wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa mwaka 2018 Runi David kutoka Shule ya Sekondari Tumbi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimvisha mmoja wa wanafunzi ambaye shule yake iliibuka mshindi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA TRA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>


Hivyo makala FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

yaani makala yote FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/fainali-za-mashindano-ya-vilabu-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA"

Post a Comment

Loading...