Loading...

Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo

Loading...
Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo
link : Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo

soma pia


Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo

Na Anna Nkinda – JKCI
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imejipanga  kutanua huduma zake  kwa kutoa  matibabu ya moyo kwa kuwafuata wananchi wenye matatizo hayo katika hospitali za kanda zilizopo hapa nchini.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na ujumbe kutoka jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing nchini China waliotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Prof. Janabi alisema Tanzania ni nchi kubwa na ina idadi kubwa ya watu hivyo basi ili huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi  ni lazima wawafuate katika Hospitali za Kanda.

“Lengo letu la baadaye ni kuhakikisha huduma tunayoitoa katika Taasisi yetu inawafikia wananchi wengi zaidi wenye matatizo ya moyo walioko mikoani pia kutoa mafunzo kwa madaktari walioko katika hospitali za Kanda kwa kufanya hivyo tutasaidia wagonjwa wa moyo kupata matibabu kwa wakati”, alisema Prof. Janabi.

Aidha Prof. Janabi alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2015 idadi ya wagonjwa wa moyo wanaokwenda kutibiwa  nje ya nchi imeweza kupungua kutoka wagonjwa 159 kwa mwaka 2012 hadi kufikia wagonjwa wawili kwa mwaka 2017.

Prof. Janabi alimalizia kwa kuzitaja changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na  kutokuwa na nafasi  ya kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa hii ni kutokana na idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka wagonjwa 100 kwa mwaka 2016 hadi  kufikia wagonjwa 300 kwa mwaka 2018 .
 Gavana wa Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing nchini China Yu Xiao-ming akimsililiza mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.  Gavana huyo pamoja na ujumbe wake walitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea zawadi ya picha ya moyo kutoka kwa Gavana wa  Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
 Gavana wa Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming akizungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya jimbo hilo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika  Taasisi hiyo  kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na  Genofeva Matemu – JKCI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Gavana wa  Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa JKCI na wajumbe kutoka China mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo

yaani makala yote Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/gavana-wa-jimbo-la-shandong-atembelea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo"

Post a Comment

Loading...