Loading...
title : IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI
link : IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI
IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewashuru wananchi kwa ushirikiano uliopelekea matukio ya uhalifu nchini kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo matukio ya matumizi ya silaha.
Akizungumza na vyombo vya habari Jijini hapa Siro amesema kuwa matukio mengi ya uhalifu hapa nchini yamepungua ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia kuondoa uhalifu nchini. Amesema kuwa Dhamana ipo kisheria na kila mmoja na haki ya kuipatahivyo inategemea na kosa ulilofanya ndio linepelekea kupewa dhamanatena kwa siku yoyote na muda wowote.
“Swala la dhamana lipo kwa mujibu wa sheria na dhamana inatolewawakati wowote ila inategemea na makosa ya mtuhumiwa”alisema siro Amesema Hali ya ulinzi na usalama hapa nchi kwa sasa ni shwari kuanzia hapa Arusha na mikoa mengine isipokuwa kwa kigoma wameongeza askari kuendelea kudhibiti matukio kwa kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa ya mipakani ina ina muingiliano.
Aidha amesema kuwa matukio ya mauaji ya mapenzi yamekuwachangamoto kubwa na yanalisumbua jeshi hilo hususani masuala ya ubakaji lazima tuwe wastaarabu kuepuka matukio yatakayopelekea mauaji na familia kuteseka. “Suala la mauaji ya wapenzi kwa wapenzi ikiwemo kufumaniana limekuwa changamoto kwetu tumejipanga kuyashughulikia na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kulishughulikia hilo lipo kwenye uwezo wao”alitanabisha Sirro
Amesema kuwa ushamba ndio unaopelekea mtu kumuua mpenzi wake hivyo kuifanya familia kuteseka na kuwasihi watanzania kuweza kuepuka matukio hayo kwa kuwa wastaarabu na kuvumiliana.
Hivyo makala IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI
yaani makala yote IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/igp-sirro-awashukuru-wananchi.html
0 Response to "IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI"
Post a Comment