Loading...
title : Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun
link : Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun
Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun
Na Raya Hamad ORKSUUUB
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman Mhe Haroun Ali Suleiman ametaka kuwepo kwa utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana juu mambo mbali mbali yanayohusu Katiba Sheria ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa
Waziri Haroun ameyasema hayo wakati alipokutana na Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisini kwake Mazizini ambapo wamekubalina kushirikiana pamoja kwa baadhi ya masuala yanayohusu na yasiyohusu Muungano
“ wizara zetu hasihusiani na Masuala ya Muungano lakini si vibaya tukawa tunashirikiana baadhi ya mambo mfano ndani ya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi mara nyingi linapokuja suala la Katiba changamoto nyingi zinajitokeza hivyo changamoto hizi zinapokuja na tukiwa na mashirikiano ya karibu hazitakuwa kikwazo ”
Zanzibar ina Katiba yake na Tanzania ina Katiba yake lakini kumekuwa kukijitokeza mijadala ya mara kwa mara hasa suala la Katiba hivyo Mawasiliano ya mara kwa mara hasa yanayohusu mijadala ya Katiba na sheria itasaidia sana kiutendaji na kiutekelezaji kwa kuondosha kasoro ndogo ndogo zilizopo na kutekeleza majukumu ya Taasisi hizi kwa ufanisi
Nae Prof. Palamagamba Kabudi ametilia mkazo baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji ushirikiano zaidi ikiwemo kushirikiana kwenye Utungaji wa sheria, mafunzo juu ya uandishi wa sheria kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambapo Zanzibar ndio kunakopatikana lugha fasaha ya Kiswahili “Watanzania wetu ni waswahili na wasomaji wetu ni waswahili ”alisisitiza waziri huyo
Aidha eneo jengine ni suala la kushirikiana katika mafunzo yakiwemo ya Mahakimu , waendesha mashtaka ambapo ameahidi kuleta watendaji ili kubadilishana uzowefu na kujifunza zaidi mbinu na mikakati katika kupata mafanikio
Prof . Kabudi pia amesifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa katika kusimamia masuala ya Katiba na Sheria na kuona umuhimu wa kuzibadilisha sheria ambazo zimeshapitwa na wakati na zile ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho .
Mawaziri hao kwa pamoja wamekubaliana kukaa na kubainisha maeneo ambayo yanahitaji kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika kwa kuwashirikisha watendaji wakuu ili wakae pamoja na kupanga mikakati endelevu ya ushirikiano ikiwemo fursa mbali mbali za mafunzo ndani na nje ya nchi , kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka Tanzania Bara kuja Zanzibar na Zanzibar kwenda Tanzania Bara .
Hivyo makala Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun
yaani makala yote Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/kuwepo-na-utamaduni-wa-kubadilishana.html
0 Response to "Kuwepo na utamaduni wa kubadilishana mawazo na kushirikiana katika mambo ya Katiba na Sheria: Waziri Haroun"
Post a Comment