Loading...
title : MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR
link : MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR
MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR
Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia
Kundi la madaktari bingwa 14 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili Zanzibar tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa siku 10. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba.
Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya tatu kufanyika Zanzibar.
Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba Iliyojulikana kama (Surgical Caravan 1) kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa. Mwezi Oktoba 2017 pia walifanya kambi ya pili iliyojulikana (Surgical Caravan 2) katika hospitali za kisiwa cha Pemba.
Katika safari yao miaka miwili iliyopita madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu kufanya kambi ya tatu (Surgical Caravan 3).
Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watasafiri na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
Viongozi wa Madaktari wa Saudi Arabia wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza walipofika Ubalozi mjini Riyadh kuaga.
Hivyo makala MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR
yaani makala yote MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/madaktari-bingwa-14-kutoka-saudi-arabia.html
0 Response to "MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR"
Post a Comment