Loading...
title : MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO
link : MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO
MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa ameweka bayana, askari wa usalama barabarani hawataona muhali kuchukua hatua dhidi ya mabasi ya abiria yatakayojaza abiria pamoja na yanayokalisha abiria waliozidi kwenye ndoo za lita 20.
Aidha ameyaasa ,magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi .
Akitoa rai hiyo kwa waandishi wa habari, Nyigesa alisema ,haiwezekani madereva wakakiuka sheria za usalama barabarani kwa makusudi wakitegemea kutoa faini bali wanachotakiwa ni kufuata sheria zilizopo.
Aliwataka ,abiria na jamii kutoa ushirikiano kwa askari hao kwa kutoa taarifa ama kuyafichua magari ya abiria yanayojaza abiria kupita kiasi ili wayachukulie hatua ikiwemo kupigwa faini.
Nyigesa alieleza, magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi . Aliwataka, waendeshaji wa vyombo vya moto kutii sheria, na kwamba magari yao yatakaguliwa yawapo ndani ya mkoa huo.
“Magari ya watoto yaliyo mengi hayana mikanda sasa ni jukumu lao kujikaguwa kabla hawajakaguliwa na kukamatwa , “Hakuna polisi atakayemuonea aya dereva wala hatutaona muhali katika suala hili la kudhibiti ajali”alisisitiza Nyigesa.
Kamanda huyo alieleza, kila mmoja atii sheria bila kushurutishwa

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Hivyo makala MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO
yaani makala yote MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/magari-ya-abiria-yanayokalisha-abiria.html
0 Response to "MAGARI YA ABIRIA YANAYOKALISHA ABIRIA WALIOZIDI KWENYE NDOO KUKIONA -RPC WANKYO"
Post a Comment