Loading...
title : MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO
link : MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO
MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO
FAMILIA ya sheikh Mohammed Ramiya, imeiangukia serikali na wizara ya utalii kuangalia uwezekano wa kuweka sehemu ya kumbukumbu kati ya hayati sheikh Ramiya na Mwl.J.K Nyerere, eneo la Zawiyani kata ya Dunda,Bagamoyo ili kuenzi historia ya ukombozi wa nchi yetu .
Aidha familia hiyo inakumbuka wakati marehemu sheikh Ramiya (78) akiugua kabla ya kufikwa na umauti wake mwaka 1985 ,Mwl. Nyerere alimchukua kumuuguza nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam .
Akizungumzia namna anavyomkumbuka hayati Mwl.Nyerere, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, mtoto wa mwisho wa sheikh Ramiya, aitwae Ramiya Mohammed Ramiya alisema ,watalii wengi wakienda kwenye makumbusho za Bagamoyo wanakuta historia ya sheikh huyo na hayati Mwl. J.K Nyerere .
Alieleza watalii hao, huwa na shauku ya kwenda kujua historia ya picha na nyumba aliyokuwa akienda kufanyiwa dua muasisi huyo ,kisha kubarikiwa kwenda kuikomboa nchi mwaka 1961.
Ramiya alisema ,enzi hizo mwalimu Nyerere alikuwa rafiki wa sheikh Ramiya ,na alipelekwa huko na wazee wa Dar es salaam kwa nia ya kuombewa dua kwa ajili ya kupata uhuru bila kumwaga damu .
"Tukiacha marehemu baba kupigania uhuru,kuheshimika lakini pia sheikh Ramiya alikuwa mtu wa dini hivyo tutapendezwa kama serikali itatambua umuhimu wa kuweka makumbusho hiyo hapa basi iwe ya kidini zaidi "
"Historia itakuwa haipotei ,lakini iwe tofauti kwa kuwa ni sehemu ya dini ,haitowezekana eneo hilo watu wakawa nje ya maadhi ya kiislamu ,isiruhusiwe wadada kwenda vichwa wazi ,ama kuvaa suruali bila kujistili " alibainisha Ramiya .
Mtoto wa mwisho wa sheikh Ramiya ,aitwae Ramiya Mohammed Ramiya akielezea namna anavyomkumbuka hayati Mwl. J. K .Nyerere huko Zawiyani ,Bagamoyo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mtoto wa mwisho wa sheikh Ramiya ,aitwae Ramiya Mohammed Ramiya (wa kulia )akionyesha historia ya nyumba aliyokuwa akienda kufanyiwa dua muasisi hayati Mwl.J.K Nyerere ,kisha kubarikiwa kwenda kuikomboa nchi mwaka 1961, nyumba ambayo kwasasa ina karne mbili , imekuwa gofu na ilijengwa kwa mawe ,(wa kushoto) ,Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo alhaj Abdul Sharif .
Jumba lenye historia aliyokuwa akienda kufanyiwa dua muasisi hayati Mwl.J.K Nyerere ,kisha kubarikiwa kwenda kuikomboa nchi mwaka 1961, nyumba ambayo kwasasa ina karne mbili , imekuwa gofu na ilijengwa kwa mawe ,ipo eneo la Zawiyani ,Dunda wilayani Bagamoyo.
Mtoto wa mwisho wa sheikh Ramiya, aitwae Ramiya Mohammed Ramiya, akionyesha historia ya picha mbalimbali baina ya hayati sheikh Ramiya na Mwl. J.K. Nyerere.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO
yaani makala yote MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/makumbusho-ya-nyerere-kufanyiwa-dua.html
0 Response to "MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO"
Post a Comment