Loading...

MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14

Loading...
MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14
link : MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14

soma pia


MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14



Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Kampuni ya Miranda Sport imeandaa tamasha la Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na wadau wengine kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki miaka 19 iliyopita.



Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo Kulwa Karedia,  alisema tamasha hilo litapambwa na mashindano ya riadha, mpira wa miguu,mashindano ya baiskeli  na mkesha wakuabudu usiku wakuamkia Oktoba 14.

Amesema kuwa tamasha hilo limepewa jina la Tamasha la Mwalimu Nyerere litashirikisha wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara ikiwemo Tarime,Bunda,Musoma,Butiama na Serengeti pamoja na mikoa jirani.

Karedia amebainisha kuwa mbio zote zitaanzia Uwanja wa Mwenge wa Butiama kupitia  Ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama kuelekea barabara ya Kiabakari ambao Mwalimu Nyerere aliutumia wakati wakuunga mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka 1967.

Amesisitiza kuwa mbio zitahusisha urefu wa kilometa 10 kwa watu wa umri wa miaka 15 nakuendelea, kilometa tano kwa vijana wa miaka 13-18, na mbio za kilometa 12.5

Karedia amesema kutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli zitakazo aanzia Butiama kupitia Buswege-Buturugi,Sabasaba,Kiabakari hadi Butiama.

Ameongeza kuwa kutakuwa na tamasha la mpira wa miguu ambapo timu tatu ambazo ni kombaini ya Butiama, Kombaini ya Wilaya ya Serengeti na mabingwa wa kombe la Siro kutoka kijiji cha kiabakari zitashiriki.

“Tumeamua kumuenzi Mwalimu kupitia sanaa za michezo kwakuwa naye alikuwa mdau wa michezo, pia tutakuwa na mkesha wakusifu nakuabudu ambapo vikundi vya kwaya vitakesha vikisifu nakuabudu usiku wakuamkia Oktoba 14,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Utamaduni wa Wazanaki, Mashaka Mgeta amewataka wakazi wa Butiama na mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi katika maadhimisho ya kumbukidhi hiyo.

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washiriki na washindi katika mashindano hayo zikiwemo seti za jezi, medali za shaba, baiskeli mpya na mipira na kiasi cha pesa ambacho kitatangazwa baadae.

Mgeni rasmi wa tamasha hilo anatarajiwa kuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa, na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ni miongoni mwa wageni waalikwa.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inasema Twende Butiama tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo.


Hivyo makala MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14

yaani makala yote MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/miranda-sport-yaja-na-tamasha-kabambe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MIRANDA SPORT YAJA NA TAMASHA KABAMBE KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14"

Post a Comment

Loading...